best

best

1 adj (independent superl) see good, 1 bora kabisa, aali, -ema sana, -ote the ~ student in the class mwanafunzi bora kabisa darasani. the ~ part of takriban, sehemu kubwa kabisa ya the ~ thing to do jambo litakaloweza kuleta mapato maridhawa make the ~use of tumia jambo fulani kwa ufanisi (mkubwa). put one's ~ foot foward kazana, fanya chapuchapu. with the ~ will kwa nia njema kabisa. ~ man msimamizi wa bwana harusi.

best

2 adv (independent superl see well, better) 1 vizuri kabisa she was the ~ dressed woman in town alikuwa mwanamke mvaa vizuri kabisa mjini. as ~one may/can kadiri inavyowezekana, kwa namna inavyowezekana. think ~ amua njia bora kabisa do as you think ~ fanya kwa namna unavyoona ni bora. 2 kabisa, sana, kuliko he is the ~ hated man in the village yeye ni mtu anayechukiwa sana kijijini. bestseller n kitabu kinachouzwa sana his new novel is one of the season's ~ sellers riwaya yake ni kitabu kinachouzwa sana msimu huu. 3 had ~ -yapasa, afadhali you had ~ come home early afadhali urudi nyumbani mapema.

best

3 n (pron.) (independent superl see better) 1 watu wenye uwezo, hadhi au sifa; -wabora he is the ~ in his profession ana uwezo mkubwa kuliko wote katika kazi yake we are the ~ of friends sisi ni marafiki sana. 2 kitu, hali, mazingira, tendo bora. be at one's ~ kuwa katika hali, afya njema. be all for the ~ kuwa na matokeo mema mwisho (ingawaje mwanzoni hapakuwa na matazamio mema). do something all for the ~ tenda jambo kwa nia njema (ingawa huenda isionekane hivyo). be/dress in one's (Sunday) ~ valia nguo nzuri kabisa. (even) at the ~ of times (hata) pale mambo yanapoitika. have/get the ~of it/of the quarrel deal/bargain shinda, nufaika, faidi. have/get the ~ of everything faidi kila kitu. with the ~ na mtu yeyote yule. with the ~ of intentions kwa nia njema kabisa. do one's ~/the ~ one can fanya liwezekanalo. make the ~of a bad bestjob/business jitahidi dhidi ya vikwazo. make the ~ of one's way home rudi haraka nyumbani licha ya matatizo. make the ~ of things ridhika (hata kama mambo hayaridhishi). to the ~ of my knowledge kadiri nijuavyo.

best

vt (colloq) shinda.