Kamusi ya TUKI Kiswahili-Kiingereza na Kiingereza-Kiswahili zimetengenezwa na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), kwa Kiingereza Institute of Kiswahili Studies (IKS), kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hapa unaweza kutumia hizi kamusi zote mbili kwa namna ya app (programu) offline, yaani inafanya kazi bila mtandao ya Wi-Fi ama data za kwenye simu. App hii inafanya kazi kwenye komputa za aina zote, tablet na simu za mkononi.
Yaliyomo ya app hii ni kutoka Kamusi ya Kiswahili-Kiingereza toleo la kwanza, mwaka 2001 iliyotengenezwa na TUKI (Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili), ambayo ilibadilishwa jina kuwa TATAKI.
Kamusi hii inatumia Kiswahili sanifu, kwa hiyo inafaa Kiswahili cha Tanzania, Kenya na nchi zingine. Kiingereza chake ni cha Uingereza. Kwa maelezo zaidi kuhusu utumiaji wa kamusi hii, rejea Mwongozo wa kutumia Kamusi.
Kupitia MobiTUKI Kamusi Kiingereza-Kiswahili utaweza:
- Kupata tafsiri kwa Kiswahili za maneno na nahau nyingi za Kiingereza.
- Kujifunza kategoria ya kisarufi ya kila neno (nomino, kitenzi…)
- Kuhifadhi tovuti hii kwenye ukurasa kaya ya simu yako na kuitumia hata bila mtandao.
Kupitia MobiTUKI Kamusi Kiswahili-Kiingereza utaweza:
- Kupata tafsiri kwa Kiingereza za maneno na nahau nyingi za Kiswahili.
- Kujifunza asili ya kietimolojia ya maneno ya Kiswahili yaliyotoholewa.
- Kujifunza vinyambuo vya vitenzi.
- Kujua aina ya neno kwa kila neno la Kiswahili, na pia vitenzi elekezi na sio elekezi.
Kupitia MobiTUKI hutaweza:
- Kupata maneno ya Kiingereza yaliyonyambulishwa (vitenzi vilivyonyambulishwa, nomino za uwingi, nk.)
- Kutafsiri sentensi nzima.
Tovuti hii haina ushirika rasmi na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili wala na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wala haiziwakilishi kwa namna yoyote.