wreck

n 1 kuvunjika (hasa chombo, merikebu, jahazi, meli), kupanda mwamba, (fig) kuvunjika kwa mipango, matarajio ya mtu. 2 meli iliyopata baa la kuvunjika. 3 gofu, chombo au jengo lililoharibiwa sana; mtu aliyetambarika vt haribu, bomoa; angamiza. wreckage n mabaki ya chombo (kilichovunjika). wrecker n 1 mtu anayelipwa kurudisha meli iliyoharibiwa. 2 mbomoaji majengo ya zamani. 3 (hist) msababisha kuvunjika kwa meli (ili apore).