way

n 1 njia, barabara. pave the ~ for andalia, andaa. The W~ of the Cross Njia ya Msalaba. 2 mapito; njia (yakupitia/kutumia). go one's ~(s) ondoka. go out of one's ~ to do sth fanya bidii kubwa, fanya jitihada maalum. lead the ~ ongoza njia, toa mfano. make one's ~ in life fanikiwa. make the best of one's ~ fanya hima, enda haraka iwezekanavyo. make one's ~ (to/ way fowards) enda, jiendea. pay one's ~ epuka madeni; jilipia gharama. the parting of the ~s (fig) njia panda. by ~ of kupitia. out of the ~ geni, tunu, sio -a kawaida, -a ajabu, miujiza. out-of-the- ~ adj (attrib) -a mbali, siofikika kwa urahisi. 3 by the ~ njiani; safarini; (fig) pamoja na hayo. on the/one's ~ njiani. on the ~ out (colloq) -nayo karibia kupitwa na wakati, nayoelekea kupoteza umaarufu. 4 njia; mkakati, mbinu. where there's a will there's a ~ (prov) penye nia pana njia. ~s and means n mbinu, njia. have/ get one's own ~ pata/tenda/ fanya mtu atakavyo; fuata njia yako. go/take one's own ~ fuata matakwa yake mtu, fanya mtu aonavyo. 5 (sing only) masafa, hatua, umbali. 6 upande; welekeo look this ~ tazama upande huu. put sb in the ~ of (doing) sth saidia mtu kuanza jambo. 7 (colloq) karibu na, upande wa. 8 maendeleo, kufuata uelekeo fulani. be under~; have ~ on (of ship) kata maji, enda. gather/lose ~ kaza/legeza mwendo; ongeza/poteza kasi. get under ~ anza kwenda, wa mbioni. make ~ (lit or fig) piga hatua. 9 nafasi/mwanya wa kusonga mbele, uhuru wa kuendelea. be/put sth out of harm's ~ wa/weka katika hali ya usalama, salimisha. get sth out of the ~ ondosha. make ~ (for) pisha. put sb out of the ~ ondoa (kwa kufunga/kuua kisirisiri); fanya atoweke. put sb in the ~ of (doing) sth saidia kuanza/kupata. see one's ~ (clear) to doing sth ona jinsi/namna ya kufanya mambo; -wa na hakika ya kufanya jambo. 10 mwenendo, desturi good old ~s desturi njema za zamani. to my ~ of thinking kwa maoni yangu. the ~ (colloq adv) kama, jinsi. mend one's ~s jirekebisha, jirudi. 11 namna. no ~ (sl) katu, hasha they are in no ~s similar hawafanani hata kidogo kwa namna yoyote ile. 12 hali in a bad ~ katika hali mbaya. any ~ vyovyote vile iwavyo. each ~/ both ~s kote kote, kila upande. have it both ~ s taka kote kote. be in the family ~ -wa mjamzito. in a big/small ~ kikubwa/ kidogodogo. 13 mwendo, utaratibu the law had its ~ sheria ilifuatwa. 14 by ~ of kwa kusudi ya; kwa namna ya. 15 (pl) ways n see sleepway. 16 (compounds) waybill n orodha ya mali ya abiria (shehena). wayfarer n msafiri (agh. kwa miguu). wayfaring adj -a kusafiri; -a kupenda kusafiri n safari. wayleave n haki ya kupita njia. wayside n kando ya njia adj kando ya njia adv mbali. ~ behind adv nyuma; kwa mbali sana ~ back in my boyhood zamani katika siku zangu za utotoni. ~ out adj (colloq) -a ajabu. waylay vt vizia we were ~laid tuliviziwa. wayward adj kaidi; tundu; tukutu. waywardness n ukaidi; utukutu.