water

n 1 maji salt ~ maji chumvi cold ~ maji baridi by ~ kwa dau/meli/boti n.k. in deep ~(s) matatani. in smooth ~ -enye kuendelea vizuri. on the ~ katika dau, meli n.k. under ~ -lio jaa maji, -liofurika. be in/get into hot ~ pata matatizo (kutokana na mwenendo mbaya). cast/throw one's bread upon the ~(s) tenda wema nenda zako (ingawa unaweza kulipiziwa baadaye). drink the ~s -nywa maji ya chemchemi kama dawa. go through fire and ~ (for sb/sth) pitia matatizo na majaribu makubwa (kwa ajili ya mtu/kitu). hold ~ (of theory etc) thibitika inapojaribiwa. keep one's head above ~ epuka matatizo ya kifedha. make ~ kojoa; (of a ship) vuja. spend money etc like ~ fuja mali, tumia, fedha kwa wingi. throw cold ~ on (a plan etc) tilia mashaka, pinga. like a fish out of ~ -enye kujisikia/vibaya kutokana na mazingira asiyozoea; -enye kujihisi ugenini/upweke. still ~s run deep (prov) kimya kingi kina mshindo mkuu; simba mwenda kimya ndiye mla nyama. written in ~ (of a name, reputation, etc) -epesi kusahaulika. the ~s of forgetfulness usahaulifu. table/mineral ~s n maji ya kunywa (yenye madini). 2 hali ya maji kupwa/kujaa. in low ~s (fig) -pungufu ya fedha, -enye fedha kidogo. 3 (pl) bahari. Tanzania. waters n bahari karibu ya Tanzania. 4 (usu pl) ziwa, mto ~s of the Nile ziwa ambalo ndio chanzo cha mto Nile. 5 kimiminiko, maji. rose ~ n maji ya waridi. 6 of the first ~ bora sana a diamond of the first ~ almasi bora sana. 7 (in compounds). water-bed n godoro la mpira lililojazwa maji. water-borne adj 1 (of goods) -a kuchukuliwa kwa meli, dau n.k.; (of diseases) -a kuenezwa na maji machafu. ~-bottle n kiriba, chupa ya maji. ~ buffalo n nyati wa kufugwa. ~cannon n bomba la maji (lenye kanieneo kubwa). water-cart n gari lenye tangi la maji ya (kunyunyizia barabarani au kuuza). ~-chute n poromoko la maji; mfereji wa maji unaotelemka. water-closet n (common abbr w.c.) choo cha kuvuta, choo cha maji. water-colour n rangi za maji; picha ya rangi za maji; uchoraji wa rangi za maji. ~-colourist n. water-cooled adj -enye kupozwa kwa maji. ~-cooler n gudulia la maji baridi. ~-course n kijito, mfereji wa maji, korongo. waterfall n maporomoko ya maji. waterfowl n ndege wa majini. ~ front n mwambao. ~ glass n ute mzito wa kukandia yai ili lisiharibike. water-hole n dimbwi, shimo la maji. water-ice n peremende barafu. ~jacket n fuko la maji la kupozea. ~ jump n kikwazo chenye mfereji wa maji (katika mashindano ya farasi). waterless adj -kavu kame, pasipo maji. water-level n kina cha maji. water-lily n yungiyungi. water-line n msitari maji: mstari ubavuni mwa meli panapofikiwa na maji. ~ -logged adj (of boat, ship, wood, etc) -liojaa maji. ~-main n bomba kubwa la kuleta maji. waterman n mwanamaji; mvushaji. water-mark n 1 kipimo cha kina. 2 (on paper) alama maalum ionekanayo kwa kuelekeza karatasi kwenye mwanga). ~ melon n tikiti maji. ~-meter n kipimamaji. water-mill n kinu cha gurudumu maji; kinu kiendeshwacho kwa gurudumu linalozungushwa na maji. water-pipe n bomba la kupitishia maji. ~ polo n mchezo wa mpira wa mikono majini. ~-power n nishati ya maji (ya kuendeshea mashine). ~-proof 1 adj -siopenya maji ~proof coat n koti (isiyopenya maji) vt fanya maji yasipenye. ~-rate n (GB) malipo ya kutumia maji. ~ -shed n eneo la mwinuko linalogawa mito; (fig) eneo la mwachano wa mambo, matukio; njia panda. waterside n ukingo. ~-skin n kiriba cha maji. ~-softener n dawa ya kulainisha maji. water-spout n 1 chamchela ya maji (hasa ya baharini); (of a roof) mlizamu. water-supply n ugavi wa maji. water-table n tabaka maji (chini ya ardhi). ~-tank n tangi la maji. ~-tap n bomba la maji. ~ tight adj -siovuja maji; siopitisha maji; (of an agreement) thabiti, -sio pindika. ~-tower n mnara wa maji. ~-wagon n gari la kubebea maji. waterway n njia ya majini. water-wheel n gurudumumaji; gurudumu lizungushwalo na maji. ~-wings n (pl) vyelezo vilivyojazwa hewa na kufungwa mabegani (ili kumsaidia ajifunzaye kuogelea). ~- works n (pl) mfumo wa ugavi wa maji; chemchem za maji zilizopambwa; (colloq) (kazi za) kibofu; (colloq) machozi. watery adj -a majimaji; chepechepe vt,vi 1 mwagia /nyeshea/nyunyizia maji. ~ing can n ndoo ya kunyweshea. ~ing cart n gari la kumwagia maji barabarani (agh kuondoa vumbi). 2 patia maji. 3 (of the eyes) jaa machozi; (of the mouth)jaa mate/maji. mouth ~ing adj -a kutia hamu sana. 4 ~ sth down tia/ongeza maji; (fig) fanya hafifu. 5 (fin) ongeza deni au mtaji wa kampuni kwa kutoa hisa mpya bila kuongeza mali. 6 watered adj (pp as adj) -liopatiwa maji, -lio na maji. ~ed silk n hariri iliyotengenezwa na kuwa na mawimbi. 7 watering place n dimbwi wanaponywea wanyama; see spa; mahali pa kupumzikia pwani.