war
n 1 vita, kondo, kitali. at ~ katika hali ya vita. carry the ~ into the enemy camp shambulia (baada ya kuridhika na kujihami/kujilinda). declare ~ (on) tangaza vita. go to ~ against anza vita (dhidi ya). have been in the ~s (colloq or hum) umia (k.m. kutokana na ajali). make/wage~ on pigana na. 2 ~ baby n mwanaharamu (wa vita) (ambaye baba yake ni askari). ~ bride n mke wa askari (aliye vitani). ~ cloud(s) n dalili za vita. ~-cry n ukelele wa kutiana shime (vitani). ~ dance n ngoma ya vita. ~ god n mungu wa vita. ~-correspondent n mwandishi wa habari za vita. ~-head n kichwa cha kombora; bomu halisi (lenye baruti). ~ horse n farasi wa vita. ~ lord n (rhet) Jemadari wa vita. ~ monger n mchochezi wa vita. W~ office n Idara ya vita. ~ paint n rangi inayopakwa mwili mzima (kabla ya kwenda vitani); (fig) mavazi rasmi ya askari; (sl) vipodozi. ~ path n (only in) on the ~ path tayari kupigana. ~ ship n manowari, meli ya vita. ~ torn adj ilioharibika na vita; -lioangamizwa na vita. ~ widow n mjane wa mwanajeshi aliyefia vitani. 3 sayansi au sanaa ya vita/mapigano/ matumizi ya silaha. 4 (fig) mapambano ~ against bribery mapambano dhidi ya hongo ~ of words mizozo. warfare n vita, mapigano; mambo ya vita. ~ like adj tayari kwa vita; nayoashiria vita; -enye kupenda vita. ~ time n wakati wa vita. warrior n (lit or rhet) mpiganaji; askari wa vita.