turn
n 1 mzunguko three ~s of the wheel mizunguko mitatu ya gurudumu. ~ of the century mwanzo wa karne mpya. on the ~ karibu ya kugeuka. done to a ~ (of food) iva/pikwa vizuri kabisa. 2 badiliko la uelekeo, kona, kuruba sudden ~s in the road kona za ghafla barabarani. at every ~ (fig) mara kwa mara. 3 badiliko la hali The sick man took a ~ for the better mgonjwa alipata ahueni. 4 zamu (ya kufanya kitu). (do something) ~ and ~ about (of two or more persons) (fanya) mmoja baada ya mwingine, fanya jambo kwa zamu. by ~s (of persons) kwa mzunguko/duru; kwa zamu. in ~ (of two persons) kwa zamu. out of ~ kabla/baada ya zamu (yako). take ~ (at something); take ~s about fanya kwa zamu, fanya kwa kupokezana. 5 tendo, kitendo kinachoathiri mtu). one good ~ deserves another (prov) matendo mema sharti yalipwe. do somebody a good/bad ~ tendea mtu wema/ ubaya; saidia/to saidia. 6 uelekeo asilia; kipaji a boy with a mechanical ~ mtoto mwenye uelekeo wa kiufundi/kipaji cha ufundi. 7 nia, matakwa, haja. serve one's ~ kidhi matakwa/haja ya mtu, faa. 8 kipindi, kifupi cha mishughuliko I'll take a few ~s before I go for lunch nitazunguka/ tembea kidogo kabla ya kwenda kula chakula cha mchana. 9 (colloq) mshituko, fadhaa, hofu it gave me quite a ~ ilinishtusha/tia hofu. 10 igizo fupi. star ~ n igizo linalopendwa sana, igizo maarufu (kwenye TV). vt,vi 1 zungusha; zunguka; pindua; pinduka; geuza; geuka the earth ~s round the sun dunia hulizunguka jua. ~ one's mind/thoughts/attention to something elekeza mawazo yako, n.k. upande fulani. ~ one's hand to something (weza ku)fanya jambo/kazi fulani. ~ a deaf ear to something -tosikiliza, -tojali. ~ somebody's flank; ~ the flank of somebody zingira ili kushambulia; (fig) shinda kwa akili; shinda katika malumbano. 2 ~ (something) (into something), geuza; geuka, badilika; badilisha. ~ somebody's brain vunga/rusha akili, tia wazimu. ~ somebody's head vimbisha kichwa. 3 fikia (kiwango fulani) na kupita he has ~ed four amefikia miaka minne, ana miaka minne sasa. 4 kereza; (fig) -pa umbo la kupendeza wood/metal that ~s mbao/chuma kinachoweza kukerezwa. 5 (of garment) shona (kwa kupindua ndani nje). ~ coat n mtu anayehama chama kimoja na kujiunga na kingine; msaliti. 6 (compounds) ~ cock n mtumishi anayefunga/fungulia maji. turnkey n bawabu; askari jela. ~ pike n (hist) lango/kizuizi katika barabara inayolipiwa ushuru wa barabara; (US) barabara inayolipiwa ushuru. ~ spit n (hist) mbwa/mtumishi anayegeuza kibanio cha nyama inayookwa. ~ table n kikalio cha sahani za santuri. 7 (special uses with adverbial particles and preps) ~ (somebody) about geuza. about ~ (as a military command, in drills, etc) nyuma geuka. ~ somebody adrift telekeza, tupa. ~ (somebody) against somebody chukiza, chochea uadui na. ~ (somebody) aside (from) (more usu ~ away) geuza mtu (aelekee upande mwingine). ~ (somebody) away geuka (upande) mtu asikuangalie; kataa (kuangalia/kukaribisha, n.k.). ~ (somebody/something) back rudisha; rudi. ~ (something) down kunja (k.m, ukosi n.k.); teremsha (k.m. utambi wa taa); punguza; pindua karata. ~ somebody/something down katalia. ~ in (colloq) enda kulala. ~ in on oneself/itself jitenga. ~ somebody in (colloq) peleka mtu polisi. ~ (something) in kunja/ingiza ndani. ~ something in (colloq) kabidhi/rudisha kwa mhusika; elekea/ elekeza ndani. ~ something off unga (bomba) zima (mitambo, redio, taa). ~ somebody off (sl) ondolea hamu/haja/nia; chusha. turnoff n kitu/mtu anayekatisha (watu) tamaa. ~ something on fungua/washa. ~ the lights on washa taa. ~ the tap on fungua bomba. ~ (somebody) on (sl) sisimua; sisimka; burudisha, furahisha. ~ on n kitu/mtu anayeburudisha/furahisha. ~on something, tegemea. ~ on somebody shambulia, chukia mtu fulani. ~ out well -wa bora mwishowe. ~ (something) out chomoza nje. ~ something out; zima/funga kung'uta (mifuko); safisha (chumba). ~ somebody/something out toa/zalisha the school has ~ed out some first-rate scholars shule imetoa wanazuoni bora. ~(somebody) out fika (kazini, kwenye shughuli, n.k.); (colloq) amsha, toka kitandani. ~ somebody out (of/from something) fukuza kwa nguvu/vitisho, n.k. ~ed out adj (of a person, equipment, etc) liovalia; liovishwa. ~ out n mahudhurio; (kipindi cha) usafi; hali ya unadhifu; mali iliyozalishwa/tengenezwa. ~ (somebody/something) over pindua; pinduka. ~ something over pata; patia; hariji his business ~s over sh 90000/= a week biashara yake humpatia shs 90000/= kwa wiki. ~ something over in one's mind fikiria/fikiri (kabla ya uamuzi). ~ something/somebody over (to somebody) kabidhi kitu/mtu fulani kwa mtu mwingine. turnover n mapato na matumizi; kiasi (cha watu, wanafunzi, wafanyakazi, n.k.) waliofika kujaza nafasi; pai yenye jamu, nyama, n.k. ndani. ~ (something/somebody) round geuza; geuka. ~ round n (esp of a ship or aircraft); kipindi cha kujiandaa na kuanza safari nyingine (baada ya kufika. ~ to fanya kazi. ~ to somebody endea au omba msaada kwa. ~ up fika, hudhuria; onekana hasa kwa bahati; (of an opportunity, etc) fika, wadia, patikana. ~ (something) up kunja (kuelekea juu). ~ up your sleeves kunja mikono yako; onyesha, weka wazi. ~ somebody up (colloq) tapisha; chafua roho. ~ up one's nose at something (fig) dharau, beza. ~ up n (for a book) tukio la kushangaza lisilotarajiwa; (of trousers) mkunjo (mguuni). ~ upon shambulia. turning n 1 kona, njia panda. ~ingpoint n 1 (fig) kipindi muhimu. 2 mahala pa kugeuka. 3 jambo kuu/muhimu.