traffic

n 1 nyendo/wendaji wa watu/magari barabarani/ ndege angani; watu, magari yanayopitapita barabarani/ndege angani. ~ circle n kiplefti, panda, kizingwa. ~indicator/ ~ator n indiketa ya gari, ishara, kiashiria. ~ jam n msongamano wa magari barabarani. ~ light(s) n taa zinazoongoza magari. 2 (biashara ya) usafirishaji watu/mizigo kwa barabara, meli, ndege na reli; mizigo, watu wanaosafirishwa kwa magari, meli, reli, ndege. 3 magendo, biashara haramu ya madawa ya kulevya. 4 wanunuzi wanaotembelea eneo la biashara. 5 mawasiliano/shughuli baina ya watu. vi ~ in something (with somebody) fanya biashara ya (na), chuuza, badilishana mali. ~er n mfanyabiashara (hasa) ya magendo. a drugs~er n muuza madawa ya kulevya.