touch

n 1 kugusa; mguso. at a ~ kwa kuguswa tu. 2 hisi ya kugusa soft to the ~ laini, nyororo. touchstone n kipimo, kigezo; kiwango. 3 rekebisho (la mwisho) final ~ es of something marekebisho ya mwisho mwisho ya jambo fulani. 4 a ~ (of) kiasi kidogo, dalili there is a ~ of hatred in his speech ipo dalili ya chuki katika hotuba yake. 5 mtindo, ufundi, namna ya kupiga/ kutengeneza kitu n.k. touch-type vi piga mashine bila ya kutazama. 6 mawasiliano, mahusiano. in/out of ~ (with) -enye kuwasiliana/ kutowasiliana na, wa/tokuwa na habari kuhusu. lose ~ (with) potezana, towasiliana. 7 (football and Rugby) nje ya uwanja. ~lines n pembe za chaki. 8 a near ~ nusura, ponea chupuchupu. touch-and-go adj (colloq) -a bahati nasibu, -a kubahatisha. 9 a soft/easy ~ (sl) n mtu aliye rahisi kuombwa au kukopwa. vt,vi 1 gusa; gusana; gusanisha; (lightly) papasa; (reach) fikia kikomo cha huzuni, n.k. ~ wood n pisha mbali. 2 (concern) pasa, husu. 3 (affect) athiri, sikitisha, huzunisha. ~ somebody on a tender place (lit or fig) gusa/umiza mtu. 4 (usu neg) -la, onja (chakula) she hasn't ~ed food for three days hajaonja chakula kwa siku tatu. 5 (equal, rival in merit) faa, shinda; lingana na; fikia no one can ~ him as a novelist hakuna anayelingana naye kwa uandishi wa riwaya. 6 (pp touched) (colloq) punguani, -enye wazimu he seems to be ~ed kama punguani/ana kichaa. 7 weza, jaribu; shughulikia she couldn't ~ the first two questions hakuweza kufanya hata maswali mawili ya mwanzo. 8 bonyeza, sukuma taratibu he ~ed the bell alipiga kengele (kwa kubonyeza swichi). 9 umiza/haribu kidogo, gusa. 10 (special uses) ~at (of a ship) tia nanga. ~ down (rugby) funga goli; (of aircraft) tua. ~ somebody for something (sl) pata fedha (agh kwa kuomba). ~ something off lipua (mzinga; n.k.); (fig) anzisha; sababisha. ~ on/upon something gusa, gusia, shughulikia jambo kwa muda mfupi. ~something up rekebisha, remba. ~ able adj -a kuweza kugusika. touching adj huzunishi, -a kutia huruma prep kuhusu, kuhusiana na. ~ingly adv. ~y adj enye hamaki, -a/-enye harara. ~ily adv. touchiness n.