throw

vt,vi 1 tupa, gea, rusha. 2 ~(on, over, off) tupia, valia; vua haraka (haraka) ~off clothes vua nguo haraka (haraka). 3 (of a rider) angusha, rusha; (of animals) zaa; (of snake) bambuka (ngozi). 4 ~(out, up, down, about) tapanya. throwaway tupa, poteza/tumia bure, fuja. throwback rejeza, rudisha. throwout toa. 5 (pottery) finyanga, umba 6. (silk) sokota. 7 (colloq) vuruga akili; sumbua, kera. 8 (sl) ~ a party fanya sherehe/ karamu/tafrija. ~ a fit shtuka/kasirika sana. 9 ~ something open (to) shirikisha kila mtu; ruhusu kila mtu kushiriki. 10 (with adv, particles and prep) ~ something about tapanya; (fig) tumia ovyo. ~ oneself at vamia, angukia; jipendekeza. ~ something away poteza (kitu) (kwa uzembe/ ujinga); tamka/sema kikawaida. throwaway n kitu kisicho na faida tena baada ya matumizi. ~ back rejea uasili/kale. ~ somebody back on/upon something lazimisha (mtu) kurudia kitu (kwa kukosa kingine). ~ down angusha; angua; (a load) bwaga. ~ oneself down jibwaga, jinyoosha chini. ~something in changia, ongeza, tia nyongeza, tia bure; (remark) ng'aka, sema; (football) rusha/tupa. a ~in n mpira wa kurusha/kutupa. ~in one's hand kata tamaa; kiri kwamba huwezi kufanya (kitu). ~ in one's lot with somebody kula bia, fanya pamoja, jiunga. ~ in the towel/sponge (colloq) shindwa; kubali kushindwa. ~ oneself into something anza kufanya kazi kwa bidii. ~ somebody/something off jikomboa, pata uhuru, ondokana na. ~ something off tunga/sanifu kwa urahisi. ~ oneself on/upon somebody/something egemea, tegemea. ~ something out tamka; (reject) kataa; (construct) ongeza/ panua, (jengo). ~ somebody out fukuza; changanya/ vuruga akili. ~ somebody over telekeza, tupa, acha, tenga. ~ something up; (resign) acha, toka, jitoa; (vomit) tapika. ~ something up tangaza, toa ilani. ~ something together kutanisha; unganisha haraka; kusanya/tengeneza haraka. ~ people together kutanisha watu. ~ up one's hands in horror nyanyua mikono kwa woga mtupo/ mrusho. within a stone's ~ (of) karibu, machoni. thrower n 1 mtupaji. 2 mtoaji.