think

vt,vi 1 (reflect) fikiri, tafakari, waza. ~ aloud toa mawazo yako (kama yanavyokujia akilini) bila kupanga. ~ tank n jumuiya ya washauri mabingwa. 2 (suppose) dhani, fikiri. 3 (neg with can/could) fikiria/elewa/jua (katika fikira). 4 dhani, fikiri I ~ I can drive well nadhani naweza kuendesha vizuri. 5 tafakari, waza, piga bongo. 6 tegemea, tarajia, kusudia, nuia. I thought as much nilitegemea hivyo. 7 (with adverbial particles and preps) ~ about something tafakari/chunguza (hasa kitu/jambo kuona uwezekano wake). ~of something fikiria, zingatia; wazia (bila kufikia hitimisho); toa wazo, pendekeza; kumbuka; wa na/kubali wazo. ~highly/well/not much/ little, etc of somebody/ something heshimu/penda/dharau/ tojali mtu/kitu. ~ nothing of something/ doing something chukulia kuwa (kitu/kufanya kitu) si kitu. ~ nothing of it usijali! ~ better of somebody heshimu sana mtu. ~ better of something achana na/tupilia mbali. ~ something out fikiria kwa makini na kufanyia mpango. ~ something over fikiria tena jambo. ~ something up buni, vumbua. n (colloq) muda wa kutafakari. thinkable adj - a kuweza kufikirika; -a kuwazika it is hardly ~able haifikiriki. thinker n mtu (wa fikara nyingi, wa akili) be a slow ~ er -wa mzito wa kufikiri. thinking n kufikiri, kutafakari; fikira, mawazo do some hard ~ing piga bongo adj -a kufikiri; -enye akili. put one's ~ing cap on (colloq) wazia, fikiria (tatizo/jambo).