talk

vi,vt 1 ~ (to/with somebody) (about/of something) sema; ongea; zungumza. ~about semea; nena; zungumzia. be ~ed about sengenywa, semwa. ~ against sema; pinga. ~ at somebody hubiri. ~ away piga porojo/gumzo. ~ back (to somebody) jibu, jibiza. ~ big jiona, ringa, piga makuu, taaradhi. ~ somebody down nyamazisha, zima; hinikiza. ~ down an aircraft elekeza rubani wakati wa kutua. ~ down to somebody sema kwa namna ya dharau. ~ing of mintarafu, kuhusu; ama kuhusu (jambo/kitu n.k. hicho). ~ in one's sleep weweseka. ~ nonsense payuka, bwata, bwabwaja. ~ round something zungumzia jambo kwa kuzunguka au bila kufikia mwisho. ~ something over zungumzia, jadili. ~ to somebody (colloq) kemea karipia. ~ing to n karipio. 2 weza kusema, sema. 3 mudu lugha, sema, tumia lugha. 4 jadili. ~ ing point n cha kuzungumzia, mada inayoelekea kuzua ubishi; wazo linaloelekea kushawishi mtu. 5 amba, nena; toboa. 6 shawishi. ~ somebody into/out of doing something shawishi/asa kufanya/kutofanya jambo. ~ somebody round/over shawishi (mtu) akubali. ~ through the nose semea puani, sema king'ong'o. ~to sema na, ongea na. 7 piga porojo; toa taarifa; iga. talkative adj msemaji, domo kaya. n msemi/ mzungumzaji; mpiga domo. n 1 mjadala; mazungumzo. 2 hotuba, mhadhara (usio rasmi). 3 (phrase) small ~ n porojo, domo. ~of the town jambo linalovuma be all ~ mazungumzo mengi yasiyo na matokeo.