take

vt,vi 1 twaa, shika. ~ hold of something shika, kamata. 2 teka; shinda; vamia ~a fortress teka boma the rat was ~n in a trap panya alinaswa katika mtego. ~cold shikwa na mafua. be ~n ill ugua, shikwa na ugonjwa. ~somebody'sfancy furahisha, burudisha. ~somebody at a disadvantage lalia, onea, endea/ shambulia mtu akiwa katika hali mbaya/ya kutojiandaa. ~somebody unawares/by surprise vamia; shtusha, shtukiza. 3 (gain, obtain) pata, jipatia; -la; nywa. ~ a bath oga. ~a holiday pumzika; enda likizo ~a meal -la ~ a deep breath pumua sana ~ pride/an interest in one's work fanya kazi kwa nia (moyo) ~ a taxi kodi teksi ~ a small house panga nyumba ndogo. 4 kubali, pata pokea I will ~ 100000 shs for it nakubali kuiuza kwa shilingi 100000 which newspaper do you ~ each day? unapata gazeti gani kila siku? ~no nonsense tokubali/to ruhusu upuuzi. ~ one's chance jaribu bahati yako. ~a chance (on something) kubali uwezekano wa kukosa. ~ it from me; ~my word for it niamini. be able to ~it; can ~it vumilia, himili. 5 ~ (down) weka kumbukumbu/andika, piga (picha) ~ (down) notes of the lesson andika kumbukumbu za mafundisho ~ a photograph piga picha. 6 (of time, need) chukua; hitaji; tumia. ~ one's time (over something) jipa muda, fanya bila haraka; (ironic) tumia muda zaidi ya ule utakiwao/ kawaida. it ~s two to make a quarrel (prov) hakuna shari ya mtu mmoja. ~ a lot of doing hitaji jitihada/ufundi mwingi. 7 (convey, conduct) chukua; peleka ~ children to the movie peleka watoto sinema; ~ home pay/wages n (colloq) mshahara (baada ya makato). 8 pima ~ temperature/measurements pima joto/saizi. 9 (use) tumia; chukua bila idhini, iba. 10 (remove) toa, ondoa. 11 fanikiwa the novel did not ~ riwaya haikufanikiwa. 12 (accept) kubali. 13 ~somebody/something for ...; ~somebody/something to be ... dhani, fikiria he was ~n for an Englishman alidhaniwa kuwa Mwingereza. ~it (from somebody) that jichukulia kuwa/kwamba. 14 ~ something as + pp chukulia (kuwa). ~something as read chukulia kuwa hakuna sababu ya kusoma. ~(it) as read that.... chukulia kwamba. 15 (with nouns) ~(a) delight/an interest/ (a) pleasure/-a pride in something furahikia/jivunia. ~an examination fanya mtihani. ~ fright (at something) ogopa, tishika. ~ a gamble (on something) bahatisha. ~somebody in hand wajibika kwake, shughulikia. ~heed zingatia, angalia. ~ a liking to penda. ~ the opportunity of doing/to do something chukua nafasi/fursa ya kufanya kitu. ~ (holy) orders wa kasisi, pata upadri. 16 ~ after somebody fanana na, shabihi, landa. ~ something apart bomoa, fungua; funua. ~ (away) from punguza; dhoofisha, fifiza. ~something/ somebody away (from somebody/ something) ondoa/ondosha. takeaway n (kitu cha) kuondoka nacho/ kulia mbele ya safari. ~something back futa (kauli); kubali kupokea/ kurudishiwa (kilichokwishauzwa/tolewa). ~somebody back (to) kumbusha/rejesha (mtu) katika mambo/kipindi cha zamani. ~ something down shusha, teremsha; bomoa; andika. ~ somebody down a peg (or two) dhalilisha, shushia hadhi; tiisha. ~something in pokea (kazi) ya kulipwa (ya kufanyia nyumbani; elewa, fahamu; ingiza, weka, -wa na.... ndani; punguza (nguo); miliki/twaa (ardhi, n.k.); chungulia, ng'amua, ona mara; sikiliza/angalia kwa msisimko; lipia na kupokea kila wakati (k.m. jarida). ~somebody in pa chumba/nyumba, pokea, laza, pangisha; ghilibu, danganya. ~ off anza kuruka; ruka. takeoff n mahala pa kuanzia kuruka; (of aircraft) kuruka/kupaa. ~something off ondoa, vua; (kettle) ipua. ~something off (something) hamisha, ondosha; punguza. ~ somebody off peleka, ongoza (njia). ~ somebody off something okoa, ondoa; dhihaki (kwa kuiga), iga. ~ off n kichekesho; dhihaka. not/never ~ one's eyes off something/somebody kodolea macho, angalia kwa makini. ~ on (colloq) sisimkwa, hemkwa; (colloq) vuma, fahamika, -wa mashuhuri. ~ something on jitwisha; geuka kuwa, chukua. ~ somebody on shindana na, -wa mshindani; ajiri; (of a bus, etc.) pakia, ingiza; pitisha kituo. ~ out something ng'oa, kamua; pata, kata; toa, ondoa. ~ out insurance kata bima. (escort) ~somebody out sindikiza, toa, fuatana na, peleka; chukua dau kubwa zaidi. ~ out a tooth ng'oa jino. ~ it out in something kubali kuchukua (kitu) kama fidia. ~ it out of chosha; dhoofisha. ~ it out on somebody tolea mtu hasira zako zote. ~ somebody over (to) vusha. ~something over (from somebody) chukua/twaa madaraka ya kitu; rithi cheo/uongozi/miliki (ya shughuli); (of Government) taifisha. takeover n badilisha uongozi/miliki ya shughuli/ kampuni. ~over (from somebody) twaa/kubali wajibu/kazi/madaraka. ~to something fanya mazoea, zoea (tabia/ mwenendo, n.k.); tumia kama njia ya kuepuka/ kutoroka; toroka, kimbia. ~ to something/somebody penda, pata tabia ya kupendelea kitu. ~something up (in the hand) inua; (of train, etc.) simama kuchukua abiria; (a liquid) fyonza, sharabu; yeyusha; (occupy) -wa kazi ya, taka, jishughulisha; fuatilia; anza upya; (time, space) chukua, maliza, bana; shika imara. ~ - up spool n kiroda cha kupokea filamu, ukanda. n.k. ~ something up (with somebody) zungumza; andikia kuhusu.... ~somebody up fanya urafiki na; saidia. ~somebody up on something kubali mwaliko/ changamoto, mwito. be ~n up with somebody/ something penda; tekwa. ~ somebody up sharp/short ingilia, katiza na kusahihisha. ~up one's residence at (formal) hamia. ~ something upon/on oneself jitolea, kubali jukumu, chukua dhima. taken adj liopatwa. be ~n by somebody's behaviour tekwa na vutiwa/zuzuliwa na tabia ya mtu fulani. taker n mwenye kupinga, mpiga-dau.