sun

n 1 the ~ n jua. rise with the ~ rauka, damka, jihimu. the midnight ~ jua kama linavyoonekana katika maeneo ya aktiki na antaktiki. 2 (the) ~ (mwanga/joto la) jua. bask in the ~ ota jua, kaa juani. under the ~ popote duniani. give somebody/have a place in the ~ (fig) -pa/wa na nafasi/hali inayoruhusu maendeleo. 3 nyota. 4 (compounds) ~ baked adj -a kuanikwa/kukaushwa juani. sunbathe vi ota jua, jianika juani. ~ beam n mwale wa jua; (colloq) mtu mchangamfu, mcheshi. sun-blind n kizuia jua (dirishani); pazia. ~-bonnet/hat n kofia ya jua. sunburn vi babuka kwa jua, badilika rangi kwa sababu ya kuungua na jua n mbabuko (unaotokana na jua). ~burnt/~burned adj -liobabuka kwa jua. ~ burst n kutokeza ghafla kwa jua. ~ dial n saa ya kivuli. sundown n 1 machweo, magharibi kuchwa (jua). ~ downer n (collq) kinywaji cha jioni; (Australia) mzururaji anayefika kwa watu jioni. ~- drenched adj -enye kupata jua sana. ~dried adj liokaushwa kwa jua. ~ flower n alizeti. sunglasses n miwani ya jua. sun-god n mungu jua. ~-helmet/hat n pama. ~-lamp n taa ya mionzi mikali kama ya jua. sunlight n mwanga wa jua, nuru ya jua. sunlit adj -a kuangazwa na jua. ~lounge/porch/ parlour n sebule (au chumba) chenye kuta za vioo kuruhusu mwanga wa jua. sunproof adj; siopenya/penywa na jua. sun-ray n mwonzi/mwali wa jua. sunrise n macheo, mapambazuko. sunroof n (or less usu ~shine roof) paa la gari lenye sehemu ya kuruhusu mwanga jua/hewa. sunset n magharibi, machweo, kuchwa. from ~set to ~rise usiku kucha. from ~rise to ~set mchana kutwa. sunshade n mwavuli wa kukinga jua; kivuli. sunshine n jua, mwanga wa jua; (fig) mchangamfu. sun-spot n (astron) alama (doa) jeusi katika jua. sunstroke n (colloq) mahali palipo na jua jingi; ugonjwa kutokana na jua kali. ~-tan n mbabuko wa jua, kugeuka rangi ya ngozi kutokana na kubabuka. suntrap n mahali penye joto na jua (bila upepo). sun-up n (colloq) macheo, mapambazuko. ~-worship n kuabudu jua; (collq) kupenda kuota jua/ kujianika juani. sunless adj pasipo jua, -a giza. sunny adj 1 -a jua. sunny side up (US) (of an egg) -liokaangwa upande mmoja. 2 (joyous) -a furaha, changamfu. sunnily adv.