spirit

n 1 roho, nafsi. the Holy ~ n Roho Mtakatifu the ~ is willing but the flesh is weak roho inataka lakini mwili ni dhaifu. 2 kivuli, mzimu, pepo. spirit-rapper n mtambikaji. spirit-rapping n kutambika kwa mizimu. 3 (fairy) mzuka, kizimwi zimwi 4 uzima (pasipo mwili); pumzi God is pure ~ Mungu ni pumzi ya uzima. 5 (always with an adj) mtu wa hekima, mwenye akili n.k. moving ~ n mwanzilishi, mtakadamu, mwasisi. 6 ari, uchangamfu, moyo (wa bidii, juhudi n.k.). 7 (sing only) hali (ya kimawazo/tabia)/moyo wa kutenda, msimamo. 8 maana, kusudi, kiini the ~ of his instructions kiini cha maongozi yake. 9 (pl) (state of mind) hali/hisia za ubongo (k.m. madadi, hasira n.k.) ya mtu in high ~s -enye furaha,. 10 (sing only) mwelekeo; hali inayoleta maendeleo the ~of the 90's mwelekeo wa miaka ya tisini. 11 ~ lamp/stove n taa/jiko la spiriti. ~-level n pima maji. 12 (usu pl) kinywaji kikali (k.m. brandi, wiski, gongo n.k.). 13 (pl) mmumunyo katika alkoholi vt ~ somebody/ something away/off torosha. spirited adj. 1 jasiri; -enye ari. 2 (in compounds) high ~ed adj -enye uchangamfu mwingi. low-~ed adj -enye majonzi. spiritless adj sio na furaha, -liokata tamaa, -zito; sio jasiri. spiritual adj 1 -a roho, - a kiroho. 2 -a pepo, -a mizimu. 3 -a kanisa; -a dini lords ~spiritual (GB) maaskofu walioko katika bunge la malodi n (Black American) spiritual n wimbo wa dini. spiritually adv. spirituality n. mambo ya roho, kuthamini mambo ya roho. spiritualism n. (imani katika) kuwasiliana na pepo (mizimu, mahoka n.k). spiritualist n mwenye kuamini kuwasiliana na mizimu/pepo. spiritualistic adj. spiritualize vt takasa, fanya -a kiroho. spiritualization n.