speak
vi sema, nena ~ Kiswahili sema Kiswahili ~ the truth sema kweli. 2 ~ (to/with somebody) (about something) sema, zungumza na, ongea na. ~ for oneself toa maoni yako, jisemea. ~ for yourself! Jisemee mwenyewe. ~ to somebody karipia, kemea, sema. ~ to something thibitisha. ~ of the devil! una maisha marefu! hufi upesi! husemwi! hutetwi! ~ with somebody zungumza/ongea na mtu. nothing to ~ of kitu kidogo tu. ~ out/up sema kwa sauti (zaidi); toa mawazo/hoja bila woga/kusita. not be on ~ ing terms with somebody toongea na mtu kwa kutofahamiana; acha kuongea na mtu baada ya/kwa sababu ya ugomvi. so to ~ yaani, kwa maneno mengine. strictly ~ ing kusema kweli. ~ing trumpet n chombo cha kusaidia kusikia. ~ ing tube n bomba la kupitisha sauti (k.m. katika meli). 3 toa ushahidi; onyesha dhahiri. ~ volumes for wa ushahidi thabiti/wa kutosha. ~ well for tetea vizuri, toa ushahidi mzuri. 4 (of language) jua, (na mudu/weza kutumia). 5 hutubia. 6 sema, toa kauli. ~ one's mind toa maoni yako ya dhati, sema bila kuficha. 7 (naut) wasiliana kwa ishara (k.m. kupungiana bendera). 8 (of a gun, musical instrument etc) toa sauti. 9 ~ easy n (US) klabu/duka la pombe haramu. speaker n 1 mzungumzaji, msemaji. 2 (abbr for loud~er) spika, kipaza sauti. 3 the ~er n Spika. speakership n uspika.