soft

adj 1 (of surfaces, of sounds etc) -ororo, laini a ~ pillow mto laini ~ wind upepo mworororo ~ fur manyoya mororo ~ music muziki mororo. ~ mud n kinamasi. ~ landing n utuaji salama. ~ land tua salama. 2 (of colours) -sio kali, -liofifia. 3 (of outlines) siokuwa wazi, -sio dhahiri. 4 (of answers, words etc) pole, -a kupendeza, tamu, laini. 5 (of water) -sio na chumvi. 6 (orig US) tamu, -si kileo. ~ drinks n vinywaji baridi. 7 -epesi, rahisi. ~ work n kazi nyepesi. ~job (sl) kazi nyepesi yenye malipo makubwa. 8 -nyonge, dhaifu. 9 -enye huruma have a ~ spot for somebody penda; pendelea. 10 (colloq) -pumbavu; bwege. 11 (compounds) soft-boiled adj liochemshwa kidogo. softcoal n mkaa hafifu (wenye kutoa moshi). ~ currency n fedha zisizobadilishika kwa dhahabu au kwa fedha fulani fulani. ~drug n dawa baridi (k.m. bangi, kungumanga n.k.). ~footed adj (of a person) -a kunyata. ~ headed adj bozi, zuzu. hearted adj -enye huruma, -pole. ~ option n njia/uteuzi rahisi. ~ palate n kaakaa laini ~ pedal (fig) lainisha (aghlabu kwa maneno). ~ soap n sabuni ya maji; (fig) kilemba cha ukoka. ~ spoken adj -enye sauti nyorororo, -enye maneno mazuri. ~ solder n lehemu/risasi laini vt lehemu/chomea na risasi laini. ~ ware n data, programu ya kompyuta. ~witted adj pumbavu. softwood n mbao laini. softish adj. softly adv. softness n. softy n 1 (mtu) bozi, zuzu. 2 (mtu) dhalili. soften vt,vi 1 lainisha, punguza (ukali), rahisisha; lainika. soften somebody up (of enemy positions) piga (kwa makombora n.k.) kabla ya kushambulia; (of persons) lainisha kwa kushawishi /kubembeleza. softener n kilainishaji.