side
n 1 upande, janibu, pembeni. other ~ of upande wa pili wa; (of river) ng'ambo ya. ~ by ~ kwa pamoja, bega kwa bega. by the ~ of; by one's ~ kandokando(ya); kwa kulinganishwa na. on/from all ~s; on/from every ~ kutoka pande zote. take somebody on one~ weka/ketisha pembeni. on the right/wrong ~ of chini/juu ya. do something on the ~ fanya kazi/mradi wa ziada kisirisiri/ kimyakimya. on the ~ pembeni. on the cold ~ baridi kidogo. lay on the ~ inika, laza kibavu. put on/to one~; (set ~) weka, tenga; (postpone) ahirisha. 2 ubavu. split/ burst one's ~s (laughing) vunja mbavu (kwa kucheka); angua kicheko. ~ splitting adj -enye kuvunja mbavu (kwa kucheka). 3 kundi; timu, chama, n.k. Tanzania has a strong ~ Tanzania ina timu nzuri. be on somebody's ~ unga mkono, wa upande/mfuasi wa. let the ~ down fanya vibaya. off ~ n kuotea. 4 (descent) nasaba, ukoo, upande on the father's ~ upande wa baba. 5 kiburi, majisifu. have no/be without ~ tojidai, tokuwa na maringo. put on ~ jidai. 6 (of animal) ubavu. 7 (compounds) ~-arm n silaha za kuvaa/kubeba ubavuni (k.m. upanga, jambia, bastola). ~-board n kabati (la vyombo) ~-burns/boards n (pl) sharafa. ~-car n kigari cha pikipiki. ~-dish n chakula cha ziada (k.m. saladi, matunda n.k.). side-door n mlango wa pembeni. ~-drum n hanzua. ~ effect n athari. ~ face adv kwa upande. side-glance n mtazamo wa chati. ~-issue n jambo dogo/lisilo muhimu. ~ light n taa ya pembeni; (fig) kiangaza: jambo lisilofungamana hasa na jambo lenyewe lakini linaliangazia. ~ -line n kazi ya ziada (isiyo ya kawaida); bidhaa za ziada; mstari wa pembeni. on the ~ lines (fig) pembeni, (kama) mtazamaji. vt zuia kushiriki mchezoni (kwa kuumia) a sore shoulder has ~ lined him maumivu ya bega lake yamemzuia kushiriki mchezoni. ~ long adj -a upande; -a kwenda upande ~ long glance tazamo la kitongotongo adv kwa kwenda upandeupande. ~ road n barabara ndogo. ~ -saddle n tandiko la farasi la mwanamke (ambalo humwezesha kuweka miguu yake upande mmoja) adv (panda) kike. side-show n onyesho dogo kwenye uwanja wa maonyesho, pambizo; shughuli/kazi ndogo. side-slip vi serereka the car ~-slipped gari liliserereka. n kuteleza, kuserereka. sidesman (church) n mtumishi/msimamizi. side-step n (hatua ya) kukwepa. vi 1 kwepea upande, epuka. ~-stroke n kuogelea kiubavuubavu. sidetrack n ujia, njia ndogo ya kando; (reli n.k.). 2 weka/pita kando; (fig) ahirisha/epa. side-view n mandhari ya pembeni. ~ walk n (US) ujia, njia (ya miguu). ~ whiskers sharafa. ~ ways/wards adv kwa upande. vi ~ with chagua upande, unga mkono.