shot

n 1 mlio, mwaliko (wa bunduki, mzinga, bastola). (do something) like a ~ (fanya) mara bila kusita/kujali, haraka. off like a ~ kwa mwendo mkali, haraka sana he was off like ~ alichomoka mbio. 2 jaribio la kupiga kitu/kufanya jambo, kujaribu kujibu swali; (in football) shuti. a ~ in the dark kubahatisha; bahati. have a ~ (at something) jaribu kufanya jambo. a long ~ jaribio la kufumbua jambo pasi kuwa na data/ushahidi wa kutosha. not by a long ~ hata kama hali ingeruhusu; hata kidogo. 3 risasi, kombora. ~put n tufe. 4 lead ~ n marisau. shotgun n bunduki ya marisau. ~ proof n siopenya risasi. 5 mpigaji (wa bunduki, picha n.k.). 6 picha long ~ picha liyopigwa kutoka mbali. 7 (US) sindano ya dawa. give/get/have somebody a ~in the arm piga mtu sindano; pa mtu uwezo wa kufufua kitu mathalani uchumi. 8 a big ~ n (slang) mkubwa, kizito aghalabu anayejivuna.