short
adj 1 (opp of long, tall) -fupi a~ while ago muda mfupi uliopita ~ steps hatua fupi. a ~ cut n njia ya mkato. ~ circuit n kosa/shoti/mkato wa umeme. vt,vi fupisha, pata shoti; (fig) fupisha, rahisisha (utaratibu). ~ list n orodha (fupi) teule. vt ~ list fupisha orodha (ya majina ya waombaji). ~lived adj -liodumu/ishi muda mfupi. a ~ range adj (of plans) -a muda mfupi; (of missiles) -a masafa mafupi. have a ~ temper wa na harara, wa mwepesi kukasirika; kuwa na hasira za haraka. ~ tempered person n mtu mwenye harara. ~term adj -a muda mfupi ~term loan mkopo wa (kulipwa kwa) muda mfupi. 2 chache, pungufu, adimu sugar is in ~ supply these days siku hizi sukari imeadimika the workers are on ~ time wafanyakazi wanafanya kazi kwa saa chache kwa siku. shortchange rudisha chenji pungufu. ~-change somebody danganya mtu (kwa kumrudishia chenji pungufu). be ~ of pungukiwa na; -wa mbali na the tyre burst when we were still ten km ~ of our home gurudumu lilipasuka km kumi kutoka nyumbani. little/nothing ~ of kama it was little ~of a miracle ilikuwa kama mwujiza. make ~ work of shughulikia haraka, fanya chapuchapu. ~of breath kuhema, kutapia hewa! shortcoming n kushindwa (kufikia lengo/kiwango kilichowekwa); dosari, kasoro. ~ drink n (or colloq); a ~ pegi ya kinywaji kikali, wiski, jini n.k.. ~ handed adj -enye wasaidizi wachache. ~sight n kutoona mbali; (fig) ujinga, kutofikiria mambo ya wakati ujao. ~ sighted adj -sioona mbali; (fig) -tofikiria mambo ya wakati ujao. ~ winded adj -enye kuishiwa na pumzi haraka; -a kutweta. 3 (in comm) -enye kupevuka/kukomaa haraka. ~ dated adj -enye kupevuka baada ya muda mfupi. ~term capital n mtaji wa muda mfupi. 4 (of a person) msema maneno machache; kusema kwa ufupi the answer was ~ jibu lilikuwa fupi/la mkato. for ~ kwa kifupi Joseph is called `Joe' for ~ Joseph huitwa Joe kwa kifupi. in ~ kwa kifupi/muhtasari. the long and the ~ of it mambo yote yapaswayo kusemwa kwa jumla. 5 (of cake, pastry) -a kuvunjika kwa urahisi. ~ pastry n (kinyunya) chenye siagi nyingi. ~ bread/cake n mkate/ keki yenye siagi nyingi. 6 (of vowels, syllables) fupi ~vowel irabu fupi. 7 (compounds) ~ fall n pungufu. ~ hand n hati mkato. by a ~ head (racing) kwa kichwa /kitambo kisichozidi urefu wa kichwa cha farasi; (fig) kwa kiasi kidogo tu. ~ horn n ng'ombe wa pembe mzingo/pinde. ~ wave n (radio, telegraphy) masafa mafupi; (kati ya mita 10 na 100). shortly adv 1 mara moja; punde. 2 kwa ufupi, kwa mkato, kwa makali. shortness n adv 1 (kwa) ghafla, mara stop ~ simama ghafla. bring/pull/take somebody up~ ingilia mtu ghafla. ~ of isipokuwa they stole all the cattle ~ of the sick ones waliwaiba ng'ombe wote isipokuwa wagonjwa tu. 2 kabla ya wakati wake (wa kawaida); kinyume cha matarajio. come/fall ~of -wa pungufu ya (matarajio) the production fell ~ of the manager's expectations uzalishaji ulikuwa pungufu ya matarajio ya meneja. cut something/somebody ~ ingilia kati, katiza, fupisha; punguza. go ~ (of) kosa, -tokuwa na, pungukiwa,wa bila you will go ~ of school fees utakosa karo. run ~ (of) ishiwa, kaukiwa the school's provisions ran ~ shule iliishiwa chakula. be taken ~ (colloq) harisha gafla. 3 sell ~ (comm) uza (bidhaa hewa/ isiyokuwepo) mapema kwa matarajio ya kununua kwa bei nafuu baadaye. sell somebody ~ saliti, danganya; dhalilisha. shortage n upungufu, uhaba; uchache there is a ~age of rice kuna upungufu wa mchele. shorten vt,vi punguza, fupisha, -wa fupi, punguka. shortening n mafuta ya kukaanga kinyunya.