shop

n (US store) 1 duka, chemist's ~ n duka la madawa. come/go to the wrong ~ (colloq) potea, topata mtu wa kutoa msaada uliotarajiwa; fika/enda mahali pasipofaa/kwa mtu asiyefaa (ili kupata msaada). keep ~ uza duka, fanya kazi dukani. keep a ~ wa na duka. set up ~ anzisha/ fungua duka, biashara ya rejareja. ~ assistant n mwuza duka. ~-bell n kengele ya duka. ~-boy/girl n msaidizi, kijana wa duka. ~ front n mbele ya duka. ~-hours n saa za mauzo. ~ keeper n mwenye duka. ~-lift vi,vt iba vitu dukani. ~-lifter n mwizi wa vitu dukani. ~ lifting n wizi wa/ kuiba vitu dukani. ~-soiled/ worn adj liochakaa (kwa kukaa sana). ~ walker n mwelekezaji (katika duka kubwa). shop-window n dirisha la kuonyesha bidhaa. put allone's goods in the ~window (fig) toa/ onyesha kila ulichonacho/ujuacho; jionyesha. 2 kazi, weledi, utaalamu. talk ~ zungumzia mambo ya kazi. shut up ~ (colloq) acha kufanya jambo. 3 kiwanda, karakana. ~-steward n mjumbe wa wafanyakazi kiwandani. closed ~ n mfumo wa uanachama wa lazima kazini. 4 all over the ~ (sl) shelabela, bila mpango, ovyoovyo, kila mahali, mahali pote. vi,vt 1 enda dukani, fanya ununuzi. ~ around (sl) enda huku na huko kutafuta bei nafuu. 2 ~ on somebody (sl) shtaki mtu. shopping n ununuzi dukani. ~ping-centre n madukani, mahali penye maduka mengi. window ~-ping n kutazama vitu dukani (bila kununua). shopper n mnunuzi, mteja.