shoot

vi,vt 1 vurumisha, vurumuiza, tupa (kwa nguvu). ~a glance at somebody tupia mtu jicho. ~ a bolt funga komeo. ~ one's bolt fanya jaribio la mwisho. ~ dice rusha dadu. (sl) ~ rubbish tupa/mwaga takataka. ~ing star n kimwondo. 2 ~ up panda sana, ruka prices shot up last month bei zimepanda mwezi uliopita. 3 (of plants) chipua, mea. 4 (of pain) choma, shambulia ghafla pain shot up my leg maumivu yamenipata mguuni. 5 (of boats) pita kasi he shot by me on the road alinipita kwa kasi barabarani. 6 piga risasi/mzinga/upinde he shot an elephant alipiga tembo risasi he wash shot three times in the leg alipigwa risasi tatu mguuni. ~ away anza na kuendelea kupiga risasi/kutupa mishale n.k.; (fig) takadamu, anza.~/get something away tapanya, sambaza, ondosha; maliza. ~ something down tungua the soldiers shot down the plane wanajeshi waliitungua ndege. ~ something off kwata (kwa risasi). ~ a covert/ an estate winda (shambani). ~ a line (US sl) ongopa, danganya, tia chumvi. ~ one's mouth off (US sl) payuka, ropoka. ~ a place up (US sl) tisha; chachafya kwa risasi na mizinga. shooting n haki ya kuwinda; eneo la kuwind(i)a. ~ing-box n banda la wawindaji. ~ing-gallery n mahali pa mazoezi ya kupiga bunduki. ~ing-party n kundi la wawindaji. ~ing-range n upigaji shabaha. ~-stick n kiti cha mwindaji: fimbo ya mwindaji ambayo pia hutumika kama kiti. ~ing war n vita hasa. 7 toa maelekezo/utaratibu wa kupiga filamu (za senema). 8 piga filamu. 9 (in sports) piga shuti. n 1 chipukizi. 2 maporomoko ya mto. 3 mahala pa kuwindia; kundi la wawindaji. shooter n (in compounds) bastola. six-~ er n bastola yenye risasi sita.