shame

n 1 haya, soni, fedheha, tahayuri It is a ~ ni aibu without ~ bila haya. for ~ aibu! ~ faced adj -enye haya nyingi. ~ facedly adv. ~ making adj (colloq) 1 -a kuaibisha wazee. 2 -a izara. bring/heap ~ on someone aibisha/fedhehesha/adhiri. 2 hizaya, fedheha, kujiaibisha. cry ~ on somebody tangaza mtu kuwa mwanahizaya. 3 utwezo, jambo la aibu. put somebody to ~ aibisha, fedhehesha. ~ on you! huna aibu, hebu ona aibu! mwana hizaya. vi,vt aibisha, tahayari(sha), tia haya, fedhehesha. ~ somebody into doing something fanya mtu afanye kitu kwa kuogopa aibu. shameful adj -a aibu, -a kutahayarisha, -a kuaibisha. shamefully adv. shameless adj sio haya, -tovu wa haya, -kavu wa macho; pujufu lead a ~less life jipujua. shamelessly adv kwa ukavu wa macho act ~lessly jipujua. shamelessness n utovu wa haya; upujufu, uchafu.