self-
pref -enyewe, -ji-, automatiki. ~-abasement n kujishushia hadhi; kujidhalilisha. ~-abnegation n kujinyima, kujitoa mhanga. ~-absorbed adj -liozamia (katika mawazo, shughuli, n.k.). ~-abuse n kujitukanisha, kujidunisha, kujidhihaki. ~-accusation n kujishtaki. ~-acting adj -a kujifanyia -enyewe; -a kujituma. ~ -addressed adj -lioandikwa anwani ya mwandikaji. ~ -activating adj -a kujiendesha enyewe. ~- adjustable adj -a kujirekebisha, -a kujirudi. ~ -admiration n kujiona; kujisifu, kujishauwa. ~-advertisement n kujionyesha, kujitangaza. ~-apparent adj wazi, bayana. ~-appointed adj -a kujiteua/ kujichagua. ~-assertion n kujitanguliza, kujitokeza. ~-assertive adj -a kujitanguliza, -a kujitokeza. ~-assurance n kujiamini. ~-awareness n kujitambua (utu, msimamo). ~-binder n mashine ya kuvunia ya automatiki. ~-centred adj -a kujifikiria mwenyewe tu, -a kimimi-mimi, -a kujipenda mno. ~-closing adj -a kujifunga -enyewe. ~-collected adj tulivu, -sio na harara. ~-coloured adj -a rangi moja. ~-command n kujitawala, kujiamuru. ~-communion n kujifikiria, kujihoji, kujitafakuri. ~-complacent adj -a kuridhika na jinsi ulivyo, -a kujiridhikia (tu). ~-complacency n kuridhika na jinsi ulivyo. ~-conceited adj -a kujipenda; -a kujiona, -a kujishauwa. ~-confidence n kujiamini. ~-confident adj -a hakika, -a kujiamini. ~-conscious adj -a kujitambua (hali, tabia, msimamo); -enye kujibaini; (colloq) -a kuona haya, -enye aibu. ~- contained adj 1 (independent) kinaifu. 2 -nyamavu, makini. 3 (complete) -a kujitosheleza, -a kujitosha, kamili; -enye yote ndani yake. ~-contradictory adj -a kujipinga. ~-control n kujidhibiti nafsi, kujiweza, kujitawala, kujizuia. ~-cooling n kujipoza. ~-criticism n kujihakiki, kujisahihisha, kujikosoa. ~-deceit n kujidanyanga, kujikanganya. ~-deception n see self-deceit. ~-defence n kujitetea; kujilinda, kujihami, kujipigania. ~-delusion n kujidanganya, kujihadaa. ~-denial n kujihini, kujinyima, kujikana, kujizuia. ~-dependence n kujitegemea. ~-desturction n kujiangamiza, kujipoteza, kujifisha. ~-determination n kujitawala, uhuru; kujiamulia (mambo). ~-display n kujishaua, kujivuna, kujionyesha, kuranda. ~-discipline n kujiongoza, kujiwekea nidhamu. ~-distrust n kutojiamini, kujihisi. -~educated adj -a kujisomesha, -a kujielimisha a ~educated teacher mwalimu aliyejifunza mwenyewe. ~-effacing adj -a kujificha, -enye soni. ~ -employed adj -a kujiajiri -a kujituma. ~-esteem n kujistahi, kujitukuza; kujiona, kiburi. ~-evident adj wazi, dhahiri, kinaganaga, bayana. ~-examination n kujichunguza, kujijaribu, kujihoji. ~-explanatory adj -enye kujieleza, -a waziwazi. ~-generating adj -a kujiongeza, -a kujizaa. ~-governing adj -a kujitawala. ~-help n kujisaidia mwenyewe, kujiweza. ~-ignition n kujiwasha. ~-importance n kujikweza, kujigamba; majivuno, makuu, kiburi. ~-important adj -a kujiona, -a kujikweza. ~-imposed adj -a kujitwisha; -a kujielemeza. ~-improvement n kujiendeleza. ~-induction n (elect.) kujichochea. ~-indulgence n -a kujiingiza/ kujishughulisha mno na mambo. ~-inflicted adj -a kujiumiza, -a kujiadhibu, -a kujitaabisha. ~-interest n umimi, uchoyo. ~-locking adj (tech) -a kujifunga. ~-made adj -liojiendeleza/-liojitajirisha enyewe. self-mutilation n kujihasiri, kujiharibu, kujilemaza, kujikata. ~-opinionated adj -kaidi, -bishi; shupavu. ~-perception n kujitambua. ~-pity n kujihurumia; kujionea uchungu. ~ -portrait n kujichora, kujichonga (kuwa katika picha/sanamu). ~-possessed adj tulivu, a kujiamini. ~-praise n majisifu; kutamba; kujigamba. ~ -preservation n kujilinda, kujihami, kujitunza, kujikimu. ~-propelled adj -a kujiendesha (kwa rada, mapanga). ~-raising adj (of flour) -enye hamira. ~-realization n kujing'amua, kujibaini. ~-recording adj -a kurekodi enyewe. ~-reliance n kujitegemea. ~-reliant adj -a kujitegemea. ~-respect n kujistahi/kujiheshimu (nafsi). ~-restrained adj -a kujikana, -a kujizuia; -a kujitawala. ~-restraint n kujitawala; kujizuia. ~-righteous adj -a kujidai; nyoofu. ~-sacrifice n kujitoa mhanga; kujitolea. ~-same adj -le -le; pacha. ~ -satisfaction n kujiona, majisifu; ukinaifu; kujiridhisha. ~-satisfied adj -a kujiona, kinaifu; -enye kiburi. ~-sealing adj -enye kujifunga -enyewe. ~-seeker n mtafuta/mtaka makuu; mwenye kujipendekeza. ~ -seeking adj -a kujipendekeza, kutafuta/kutaka makuu. n kujipendekeza. ~-service n kujitumikia, kujihudumia. ~-sown adj kimelea (-siopandwa), maotea. ~-starter n stata, kijianzishi. ~-styled adj -enye kujiita. ~-sufficiency n 1 utoshelevu. 2 kujitegemea. ~-supporting adj -a kujikimu, -a kujitegemea. ~-taught adj -liojielimisha; -liofunzwa na ulimwengu. ~-will n ukaidi, ushupavu. ~-winding adj (of watch, clock etc) -a kujilisha, -a kujitia ufunguo. ~-hood n ubinafsi, upeke. ~ish adj -a choyo, -enye ubinafsi. ~ishness n ubinafsi, uchoyo. ~ishly adv.