sea

n 1 the ~ bahari. go to ~ safiri kwa meli; -wa safari ya chombo, anza kuondoka bandarini/pwani. on the ~ (of a place) pwani. beyond/ over the ~s ng'ambo. the high ~s bahari ya mbali. the freedom of the ~s haki ya kufanya biashara katika eneo lolote la bahari. the Red S~ Bahari ya Sham. the Seven S ~s n (poet) bahari zote. 2 (various phrases without articles) at ~ baharini; -sioelewa. all/completely at ~ liochanganyikiwa. by ~ kwa meli. 3 (wave) wimbi. heavy ~ n mawimbi makubwa. 4 half ~s over -levi, wingi wa. ~ of troubles shida nyingi. 5 (attrib and in compounds) ~ air n upepo wa bahari. ~ animal n mnyama wa baharini. ~ bathing n kuoga baharini/kuongelea baharini. ~ bed n chini ya bahari. ~ bird n ndege waishio karibu na bahari. ~ board n eneo la pwani; ufukwe. ~ boat n mashua. ~ borne adj -liobebwa na meli. ~ breeze n upepo wa bahari. sea-coast n pwani, ukingo wa bahari. ~ cow n nguva. sea-dog n aina ya sili; baharia mkongwe. ~ eagle n kwazi. ~ farer n baharia. ~ faring n safari baharini adj -a bahari; -enye kufanya kazi/kusafiri baharini. ~ faring men n wanamaji, mabaharia. ~ fish n samaki wa bahari/wa maji ya chumvi. ~ food n vyakula vya habarini. ~ front n upande wa mji uliokabiliana na bahari. sea-girt adj (poet) -liozungukwa na bahari. ~ going adj 1 (of ships) -a kuvukia bahari. 2 (of person) -a ubaharia. ~ -green n kijani bahari adj -enye rangi ya bahari. ~ -lion n sili mkubwa wa bahari. ~ man n baharia. ~ manship n ustadi wa ubaharia. ~ mile n maili ya majini (futi 6080). ~ plane n ndege ituayo baharini/ziwani. ~ port n (mji wenye) bandari. ~ power n nguvu (ya jeshi la maji) ya kutawala bahari. sea-rover n haramia; meli ya haramia. ~s cape n mandhari ya bahari. seashore n ufuko. ~ sick adj -a kichefuchefu cha baharini. ~ sickness n kigegezi. seaside n pwani, ufukoni. ~snake n nyoka wa baharini. ~-view n mandhari ya bahari. seawall n ukuta/boma la kuzuia bahari. seawater n maji ya bahari, maji ya chumvi. seaway n njia ya majini; mto unaopitika na meli za baharini. seaworthy adj (of a ship) -a kufaa kusafiri baharini.