run
run
1 vt,vi 1 kimbia; kimbiza take a ~ ning jump kimbia na kuruka; (sl) ambaa; usiwe mpuuzi! 2 epuka, toroka, kimbia. ~ for it kimbia (ili kukwepa jambo). cut and ~(sl) toroka. a ~ning fight n mapambano ya manowari (kati ya wanaorudi nyuma na wanaowakimbiza). 3 shiriki katika mbio/mazoezi ya kukimbia. also ran n mshinde. 4 ~ for gombea (uchaguzi, cheo, n.k.). 5 sababisha kukimbia/kushiriki (katika mashindano ya mbio); wasilisha/teua (kushika cheo). 6 sababisha kufikia hali fulani/mahali fulani (kutokana na kukimbia). ~ somebody clean off his feet/ legs (colloq) shughulisha hadi kuchosha kabisa. ~ oneself/somebody into the ground jichosha/chosha (mtu) kwa kazi/mazoezi magumu. 7 enda haraka. ~ its course kua, endelea kawaida; fuata mkondo wa kawaida. ~ the streets (of children) cheza barabarani (bila usimamizi). 8 jiweka wazi; jihatarisha. ~ the danger/ chance of something jiweka katika hali/hatari ya. 9 kimbiza; shindana na. ~ somebody/something to earth fuatilia hadi kupata/kushika. ~ somebody/something close/hard karibia sana (katika mashindano). 10 (of ships, etc) enda safari; (of fish) ogelea. 11 (of machines) fanya kazi. 12 enda mbele kwa mwendo wa kuteleza au kuendelea; enda kama kwamba uko kwenye magurudumu. 13 (of public transport) pita; enda na kurudi (kila mara). 14 chukua (mtu katika gari, basi, n.k. na kumpeleka mahali). 15 peleka, safirisha. ~ errands/messages peleka ujumbe. ~ arms/guns ingiza silaha nchini kwa siri, fanya magendo ya silaha. ~ liquor fanya magendo ya vileo. 16 fanya kusogea au kupanuka kuelekea upande fulani. 17 (of fire, news, emotions, etc) enea haraka. 18 (of liquids) tiririka; churuzika; lowa. 19 fanya kumwagika/tiririka; fanya kuenea. 20 -wa/pitia katika hali fulani. ~ riot fanya fujo na ghasia; (of plants) enea ovyo. ~ wild kaa/kuwa bila mipango/nidhamu. ~ a temperature -wa na homa. 21 endesha, ongoza, simamia. ~ a company endesha kampuni. ~ning costs n gharama za uendeshaji. ~ the show kuwa bosi katika kadhia fulani. 22 (of thoughts, feelings memories, the eyes, etc) pitia/pitisha mara moja/kwa haraka. 23 endelea/ endelezwa katika mpango maalumu a scar that ~s across his cheek kovu linaloanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa shavu lake. the ~ning commentary n tangazo mfululizo. 24 -wa na mwelekeo fulani (wa kitabia), -wa na bei ya wastani; -wa na kiwango cha wastani. 25 (of colour) -sambaa toka sehemu yenye rangi hadi isiyo na rangi 26 andikwa, simuliwa au semwa the story ~s that hadithi imeandikwa/yasemwa kuwa ---. 27 (of woven or knitted material) fumuka. 28 (in special uses) ~ about kwenda huku na huko. run-about n motokaa ndogo (k.m. ya watu wawili); mtu atangatangaye kutafuta mambo mageni, raha, n.k. (hatulii katika sehemu moja). ~ away kimbia; jaribu kutoroka. runaway n mtu/farasi atorokaye. ~ away with tumia; toroka; iba; shinda vibaya sana washindani wengine; kubali wazo harakaharaka, fikia hitimisho lisilo na msingi; enda kwa kasi kubwa isiyodhibitika. ~ back rejea nyuma (katika mawazo). ~ down (of a clock or other mechanism of the like) simama (kwa kukosa kulishwa); (of a person's health) nyong'onyea, zidi kuwa mbaya (kwa sababu ya kazi nyingi, fikra nyingi, n.k.); (of a battery) isha; gonga/gongana; sema vibaya (mtu au kitu); fukuza na kupita/kamata; punguza nguvu. run-down n (colloq) upunguzaji orodha/maelezo kamili. ~ in tembelea (mtu mahala) kwa muda mfupi; (colloq of the police) kamata, bamba; endesha kwa uangalifu kwa mara ya kwanza (gari/mashine mpya) kwa muda/umbali fulani ili kuiweka katika hali nzuri ya matumizi. ~ into gongana; sababisha kuingia katika (deni, ugomvi, n.k.). ~ off toroka (na); churuzika/tiririka (kutoka sehemu hadi sehemu); fanya kuchuruzika/kutiririka; andika au soma kwa ghibu (moja kwa moja bila kusita/kwa ufasaha); chapa; toa (makala/kitabu); amua baada ya watu kufungana baada ya majaribio; anzisha (k.m. mbio). ~-off n uamuzi mkata. ~ something on unganisha/endeleza/ endelea; sema mfululizo; (of time) pita, isha time ~s on wakati unapita; (of disease) endelea kutokea/ kusumbua. ~ on/upon something (of thought etc) husika na. ~ out toweka; fikia mwisho, isha; (of tide) kupwa. ~ out of (of tide) kupwa. ~ oneself out of breath jichosha. ~ out on somebody telekeza. ~ over (of a vessel or its contents) furika; pitia (ili kuzingatia au kushika akilini barabara); soma harakaharaka; gonga/kanyaga mtu (kwa gari); tembelea kwa muda mfupi. ~ through pitisha msitari (k.m. katika maneno yaliyoandikwa); choma kwa singe; tumia vibaya (bahati, fedha); chungua kwa haraka; shughulikia kwa haraka; (of play) fanya mazoezi. ~ to fikia; tosha/tosheleza. ~ to fat nenepa mno! ~ to ruin haribika. ~ to waste tumika vibaya. ~ up inua, simamisha (k.m. bendera kwenye mlingoti); jenga/ tengeneza harakaharaka; fanya kuongezeka kwa haraka; fikia kiasi cha/pata/ongeza mwendo kimbia (kabla ya kutupa mpira, mkuki, n.k.).run
2 n kukimbia. ~up n 1 urefu (wa kukimbia), masafa; kipindi kabla ya tukio kubwa. a ~ for one's money malipo ya kazi au juhudi za mtu; -pa ushindani mkubwa. 2 ziara, matembezi a ~ to Mikumi ziara ya Mikumi. 3 (of a ship) umbali (wa mwendo kwa kipindi maalumu). 4 njia (ya mashua, meli, n.k.). 5 mshuko wa ghafula price came down in a ~ bei zilishuka kwa ghafla. 6 mfululizo wa maonyesho (k.m. ya muziki, tamthiliya, n.k.). 7 kipindi; mfuatano a ~ of bad luck kipindi cha mkosi. a ~ on something, kitu kinachohitajiwa ghafla na watu wengi. in the long ~ hatimaye. 8 (of domestic animals) zizi, banda. 9 (cricket and baseball) pointi. 10 kawaida, mwelekeo, utaratibu the common ~ of mankind watu wa kawaida. ~-of-the mill kawaida, wastani. 11 kundi la samaki wakiwa katika mwendo. 12 (colloq) give somebody/get the ~ of something ruhusa ya mtu kutumia kitu bila kulipa. 13 mwelekeo. 14 (music) mfuatano wa nota zinazoimbwa/ zinazochezwa haraka na kufuata daraja mbalimbali. ~ ner n 1 mkimbiaji. ~ner -up n mshindi wa pili katika mashindano. 2 (messenger) mjumbe, tarishi. 3 (surface root) kitawi cha mmea utambaao chini. 4 (plant) mtambaazi. 5 (cloth) kitambaa kirefu, kipambo cha meza. 6 (in compounds) mfanya biashara ya magendo. gun ~ner n mfanya biashara ya magendo ya bunduki. running adj 1 -a kukimbia. 2 (successive) moja kwa moja, -a mfululizo ~ning fire mfululizo wa bunduki/wa mizinga. 3 (after a pl n) katika mfuatano six days ~ning siku sita mfululizo/moja kwa moja. 4 (of water) -a kuchuruzika. 5 (discharging) -a kutoka usaha. n 1 mbio, kukimbia, kwenda mbio. make the ~ning ongoza mbio. take up the ~ning ongoza (baadaye) katika mbio. in/out of the ~ning (of competitions) -enye/ pasipo nafasi ya kushinda. 2 ~ning-board n (old fashioned) sehemu ya kukanyagia, kuingia garini. ~ning mate farasi wa kuongoza mwendo; (US) mgombea umakamu wa rais.