round
adj 1 -a duara, -a mviringo, -a kuviringa(na). a ~ game n mchezo usio na timu au idadi maalumu ya wachezaji. 2 -enye kufanywa kwa kuzungukazunguka/kuzungu-shazungusha. ~ brackets n mabano upinde. ~ dance n ngoma ya kucheza katika duara. ~ robin n barua ya maombi/malalamiko yenye sahihi zinazofanya mviringo (ili kuficha ni nani aliyeanza kutia sahihi). ~ trip n safari ya kwenda na kurudi. 3 kamili, -ote; nzima. in ~ numbers/figures namba za makumi 10, 100, 1000. 4 wazi, dhahiri, kamili. 5 (with compounds) ~ arm adj -a usawa wa bega. ~backed adj -a kibiongo. ~eyed adj kodozi; -enye macho makubwa. ~ hand n mwandiko wa herufi za kuumba. round-house n (hist) gereza; (naut) chumba cha staha; karakana ya garimoshi. ~ shouldered adj -enye matao. vt,vi 1 fanya/-wa mviringo, viringisha. 2 zunguka. 3 ~ something off kamilisha jambo. ~ out viringisha. ~ somebody/something up leta pamoja, kusanya. ~ up (a figure/ price) fanya (idadi) kamili. a ~ up msako. ~ on (upon) geuka ghafla. ~ upon somebody geukia mtu na kumshambulia (kwa maneno au kwa vitendo). n 1 kitu kilicho na umbo la mviringo. 2 (of sculpture) umbo linalokiwezesha kitu kuonekana kutoka sehemu zote. in the ~ (arts) -liotengenezwa/fanywa ili kuonekana pande zote. theatre in the ~ jukwaa linalozungukwa na watazamaji. 3 (series) mfululizo, mfuatano, mgawo, mzunguko. make one's ~s fanya raundi za kila siku/mara (k.m. kukagua). go the ~ of; go the ~s fikia (watu, mahali), sambaa, enea haraka the news went the ~ of the school habari zilisambaa haraka shuleni. 4 (games contest, etc) raundi the third ~ of the super league raundi ya tatu ya ligi kuu; duru. 5 mzunguko (wa kitu kinachogawiwa watu, k.m. kwenye unywaji wa pombe). 6 wimbo wa kupokezana. 7 mchezo wa dansi ambapo wachezaji hucheza katika mtindo wa duara prep 1 (expressing movement) kwa kuzunguka. sleep/work ~ the clock (attrib) lala/fanya usiku na mchana, saa zote. 2 (expressing movement) katika njia ambayo inabadili uelekeo kutoka upande mmoja wa kitu hadi upande mwingine. ~ the bend (sl) kichaa. 3 (expressing position) kuwa katika pande zote za kitu they were sitting ~ the table walikuwa wamekaa kwa kuzunguka meza. 4 katika sehemu mbalimbali/zote. show ~ tembeza. ~go tembelea; zunguka. 5 sehemu mbalimbali kutoka kituo maalumu. 6 ~ (about) (fig) takribani adv 1 katika duara; kwa kuzunguka. 2 kwa kurudia mahali ulipoanzia. ~ and ~ kwa mizunguko kadhaa. all ~; right ~ kwa kuzunguka kabisa. all the year ~ kwa mwaka mzima. 3 kwa kuzunguka, katika mzingo. 4 ili kuwa katika duara. 5 kutoka sehemu/ eneo/mtu mmoja hadi mwingine. hand ~ gawia/mpe kila mmoja. go ~ tosheleza. taking it all ~ kwa kulitazama (k.m.) katika ujumla wake/pande zake zote. look ~ tembelea. 6 kwa kutumia njia ndefu zaidi. 7 kwenye sehemu alipo mtu/atakapokuwa mtu. 8 ~ (about) jirani/katika mazingira jirani. roundly adv sana, wazi. roundabout adj -enye kuzunguka. in a ~about way kwa kuzungukazunguka. n 1 pembea. you lose on the swings what you make on the ~abouts (prov.) kata pua uunge wajihi. 2 kipulefti, kizingwa, kisiwa (cha trafiki).