roll

vt,vi 1 bingirisha; bingirika heads will ~ (colloq) watu watafukuzwa/ umbuka. 2 ~ (up) sokota; kunja, zongomeza ~ a cigarette sokota sigara. 3 enda, pita the clouds ~ed away mawingu yalitoweka tears ~ed down his cheeks machozi yalimtiririka. 4 geukageuka. 5 (make flat) tandaza; sukuma (k.m. chapati); futa; nyosha. ~ed gold n tabaka nyembamba ya dhahabu (juu ya metali nyingine). 6 sukasuka, yumbayumba. 7 (of surfaces) tia mawimbi. 8 (of waves) panda na kushuka. 9 nguruma ~ one's r's sema kimadende. 10 ~ at (of eyes) geuzageuza, zungusha. 11 rolling n (compounds) ~ing mill n kiwanda cha kusukuma metali. ~ing pin n kijiti/ mpini/kipande cha kusukuma unga. ~ing stock n mabehewa, mabogi ya reli. 12 (with adv particles and prep) ~ something back rudisha nyuma (k.m. adui). ~ in miminika, wasili/fika kwa wingi. be ~ing in jaa they're ~ing in money wamejaa. ~ on pita; fika haraka. time ~ed on wakati ulipita. ~ on the weekend! wikendi ifike haraka. ~ something on vaa nguo kwa kuzungusha kwenye miguu. ~ something out tandaza. ~ out the red carpet (fig) -pa mgeni rasmi makaribisho makubwa; (of pastry etc) sukuma. ~ up (of a vehicle) fika na kusimama. R~ up! R~up! Njoo! Njoo. ~ something up (mil) rudisha nyuma. ~ n 1 kitu chenye umbo la mcheduara (kutokana na kuviringwa; (of cloth) jora (of paper) gombo; (of film) filamu; (of tobacco) bumba; (of bread) skonzi. ~ top desk n deski lenye mfuniko unaokunjika. 2 ukingo uliogeuzwa (k.m. pindo la nguo lililogeuzwa). 3 mwendo wa kubingiria. 4 orodha rasmi (hasa ya majina). ~call n kuita majina (ya wanafunzi, askari, n.k.) katika orodha. ~ of honour n orodha ya majina ya watu waliokufa kwa ajili ya nchi yao. strike off the ~s ondoa jina la mwanasheria katika orodha ya wale wanaoruhusiwa kufanya kazi ya uanasheira. 5 sauti ya mbingirio, ngurumo. roller n 1 chuma/mti/mpira - mcheduara (-a kukandamizia, n.k.). 2 rola: gurudumu aina ya mcheduara. ~er skates n rolasketi: magurudumu yanayofungwa chini ya kiatu/ubao kwa ajili ya kutelezea. 3 ~er bandage n bandeji ya operesheni. 4 wimbi refu na kubwa.