register

n 1 rejesta, daftari yenye rekodi. 2 kadiri ya sauti. 3 chombo (mashine) cha kuonyesha na kurekodi kasi, kani, namba. 4 kirekebishi (cha kupanua au kupunguza ukubwa wa tundu, uwazi, n.k.). 5 (gram) rejista: lugha itumikayo katika muktadha maalumu. 6 see registry n. ~ (something/oneself) (with something/somebody) (for something) vt,vi 1 sajili, andikisha, rajisi ~ voters andikisha wapiga kura ~ an association sajili chama. 2 onyesha (hisia, kiasi cha joto, hali, n.k.) his face ~ed anxiety uso wake ulionyesha wasiwasi the thermometer ~ed 40 degrees centigrade pimajoto ilionyesha nyuzi 40 sentigredi. 3 tuma barua ya rejesta. registrar n 1 msajili, mrajisi the registrar's office ofisi ya msajili registrar of companies msajili wa makampuni registrar of societies mrajisi/msajili wa vyama. registrar-general n mrajisi mkuu. registration n 1 usajili, uandikishaji registration of deaths usajili wa vifo registration plate bamba la namba (ya kusajiliwa) ya gari. 2 ingizo; rekodi ya mambo. registry n 1 usajili central registry usajili mkuu. 2 ofisi ya msajili marriage registry ofisi ya msajili wa ndoa. 3 (also register) masijala.