raw

adj 1 bichi, -siopikwa. 2 ghafi ~ materials mali ghafi: vitu vya kufanyizia vitu vingine, k.m. pamba, katani, manyoya, mbata. in the ~ ghafi; -siyosafishwa/tengezwa; (fig) uchi. ~-hide n (-liotengenezwa kwa) ngozi ghafi. 3 (of persons) -sio na ujuzi/uzoefu a ~ recruit askari mpya asiyefundishwa bado, kuruta. 4 (of weather) -enye unyevuunyevu; baridi. 5 (of wounds) bichi, -enye damu; (of a place on the flesh) -liochunika ngozi. raw-boned adj -enye mfupa mkubwa na nyama kidogo; mifupa mitupu. 6 (artistically crude) changa his literary style is still rather ~ mtindo wa maandishi yake bado ni mchanga. 7 (colloq) kali, -onevu. a ~ treatment; ~ deal n uonevu ubichi katika ngozi (agh. ya farasi). touch somebody on the ~ (fig) tonesha, umiza, tonesha hisia za mtu.