point

n 1 ncha kali (ya kalamu, pini, kisu, n.k.). not to put too fine a ~ on it kusema ule ukweli. 2 ncha- chonge. 3 nukta (ifanywayo na kitu, kama vile kalamu). decimal ~ n desimali four ~ six nne nukta sita (4.6). 4 alama (halisi au ya kufikirika) ya eneo, mahali au wakati. a ~ of view mtazamo. (US) at this ~ mahali hapa; sasa, wakati huu. be at the ~ of death -wa mahututi. be on the ~ of doing something karibia kufanya jambo fulani. if/when it comes to the ~ wakati ukifika. ~ duty n zamu ya polisi wa usalama barabarani katika kituo maalum. 5 (printing) kizio cha kupimia ukubwa wa herufi. 6 alama (kwenye skeli); kizio cha kupimia, kiwango. boiling ~ n kiwango mchemko. possession is nine ~s of the law hamadi kibindoni. 7 pointi, alama, kizio cha kupatia pointi katika mchezo. win/be beaten on ~s shinda/shindwa kwa pointi. 8 (of compass) alama, nyuzi. 9 wazo (kuu/kiini), jambo. carry/gain one's ~ shawishi mtu akubaliane na wazo lako. come to/get to/reach the ~ sema kile (hasa) unachotaka kusema. get/see/miss the ~ pata/ ona/shindwa kuona ambacho mtu anajaribu kusema. make one's ~ jenga hoja. make a ~ of doing something chukua kitu kuwa muhimu au cha lazima kufanya. stretch a ~ kwenda mbali zaidi ya kiwango kinacho ruhusiwa.take somebody's ~ elewa/kubaliana na kile asemacho mtu. (get/wander) away from/off the ~ sema kitu kisichohusiana na habari isemwayo. a case in ~ jambo/ mfano halisi mmojawapo. in ~of honour/ conscience kitu muhimu kwa dhamira/hadhi ya mtu. 10 sababu no/not much ~ in doing something hakuna sababu ya msingi (ya kufanya kitu fulani). What's the ~ Ya nini? usihangaike bure. 11 sifa. 12 soketi/njia ya kupitia umeme. 13 maungio (ya kubadilishia njia ya reli). ~s man n mlizi wa njia panda ya reli. 14 umuhimu. vt,vi 1 ~ (to) elekeza; onyesha sehemu/uelekeo wa. ~ something at/ towards elekeza, lenga. 2 ~ something out onyesha. 3 tia nukta; (fig) kazia, sisitiza. 4 kazia maungio ya matofali yaliyojengwa. 5 (of a dog) jiweka tayari. pointed adj 1 liochongoka, -enye ncha kali; (fig) lioelekezwa dhidi ya mtu fulani. 2 (fig) -a wazi, -liolenga wazi. 3 kali. ~ edly adv. pointer n 1 mshale, akarabu. 2 fimbo (fito) ya kuelekezea/kuonyesha. 3 mbwa wa kuwinda, mwepesi kuonyesha alipo ndege au mnyama. 4 (mil) mlenga shabaha/mzinga. pointless adj 1 (fig) -sio na maana/sababu a ~less speech hotuba isiyo na maana. 2 (sport) -sio na pointi. pointlessly adv. point-blank adv 1 (of a shot) papo kwa papo; kulengwa/pigwa kwa karibu mno. 2 kinaga- ubanga, waziwazi. adj -a papohapo, -a wazi. pointillism n uchoraji wa kutumia nukta; utonaji.