play

n 1 mchezo.a ~ on words kucheza na maneno. child's ~ n kitu cha kawaida na rahisi. ~ boy n mpenda sana starehe. ~ fellow/mate n mwenzi (katika mchezo). ~-ground n kiwanja cha michezo. ~-pen n sanduku/tenga (ambamo mtoto huweza kuachwa akacheza). ~ room n chumba cha michezo ya watoto. ~-school group n vichekechea: kundi la watoto wachezao pamoja chini ya uangalizi maalum. ~-suit n nguo za kuchezea. plaything n (fig) mtu anayechezewa. ~ time n muda/ kipindi cha kucheza, mapumziko. 2 kucheza, namna ya kucheza mchezo. in/out of ~ ndani/nje (ya uwanja). fair ~ n (fig) usawa, haki kwa wote. foul ~ n kinyume na sheria; (fig) njama. 3 zamu katika mchezo it is John's ~ ni zamu ya John. 4 kamari. 5 tamthilia. as good as a ~ -a kufurahisha, -a kupendeza, senema ya bure. ~ acting n kuigiza tamthilia; (fig) kujisingizia. play-bill n tangazo la (tamthilia, mchezo n.k.). playgoer n mpenda kutazama tamthilia. playhouse n jumba la kuonyeshea tamthilia. ~ wright n mwandishi wa michezo ya kuigiza. 6 mwendo mwepesi. 7 nafasi ya kufanya jambo allow full ~ to one's ability toa nafasi ya kutumia uwezo wake. 8 kazi, kitendo, shughuli. be in full ~ tumika kikamilifu. bring something into ~ anza kutumia/kutumika. come into ~ anza kufanya kazi, anza kushughulika. vt,vi 1 cheza. ~ with jifurahisha. 2 ~ at something/being something) jifanya kuwa unafanya kitu; fanya mzaha. 3 ~ a joke/ prank/trick (on somebody) hadaa; tania. 4 shiriki katika mchezo; cheza he ~s football for our club huchezea mpira klabu yetu. 5 ~ (as/at) shika nafasi fulani katika mchezo Juma ~s in goal/as goalkeeper Juma hushika nafasi ya mlinda mlango. ~ somebody as/at ingiza katika timu. 6 (cricket, football etc) piga/gonga mpira kwa namna maalumu. ~ ball (with) (fig,colloq) -wa tayari kufanya kwa ushirika; shirikiana. 7 (of chess) sogeza (kete); (of cards) cheza (karata). ~ one's cards well (fig) tumia nafasi yako vizuri/vibaya. 8 ~ fair fuata kanuni/ sheria; fanya kama inavyotakiwa. ~ hard cheza kwa bidii. ~ the ball, not the man cheza mpira usipige watu; (fig) wa mwaminifu na kutenda haki. ~ the game fuata sheria za mchezo; (fig) -wa mkweli bila upendeleo; fuata haki. 9 piga chombo/ala ya muziki, fungua chombo cha muziki k.v. santuri ~ the flute piga zumari. ~ (something) back piga kanda baada ya kuirekodi. ~ back n chombo kinachorudisha nyuma kanda iliyorekodiwa; kurudisha nyuma kanda. 10 igiza tamthilia, onyesha maigizo. ~ the fool fanya mambo kijinga. ~ the man fanya mambo kiume. 11 yumba-yumba, wayawaya, chezacheza. 12 endesha/enda kwa mfululizo. 13 ~ (something) on/upon something piga risasi. 14 ~ a fish chosha samaki kwenye mshipi. 15 (special uses) ~ down to somebody zungumza kwa kujishusha (ili mtu asijihisi mnyonge na akuunge mkono). ~ something down dhalilisha/dunisha kitu kwa makusudi, punguza umuhimu wake. ~ somebody in, ~ somebody into a place pigia muziki wakati wa kuingia. ~into somebody's hands/the hands of somebody jiingiza/ jiuza/pa faida. ~ one person off against another gonganisha/ chonganisha. ~ (something) off n mchezo wa marudiano. ~ on upon (something) chochea. ~something out fikia kikomo/ kilele. be ~ed out kwisha; pitwa na wakati. ~up cheza kwa nguvu; (colloq) wa mtukutu. ~something up tukuza; taaradhi. ~ up to somebody jipendekeza. ~ (somebody) up (colloq) pa taabu, taabisha. ~ with chezea. player n 1 mchezaji. 2 (arch) mwigizaji. 3 mpigaji kinanda n.k.; rekodiplea, santuri. playful adj cheshi, -a kucheza, -a mzaha,-purupuru. playfully adv. playfulness n. playing n. ~ ing field n kiwanja cha michezo. playlet n tamthilia fupi.