place

n 1 mahali. 2 jiji, mji, kijiji n.k.. go ~s (colloq) fanikiwa zaidi na zaidi. ~ name n jina la mahali k.v. mlima, mji. 3 jengo/sehemu maalum. 4 ukurasa/sehemu katika maandishi. 5 cheo, daraja. keep one's ~ jua nafasi yako; heshimu wakubwa. 6 nafasi ya kitu au mtu (kati ya washindi). 7 hatua (katika majadiliano n.k.). in the first/ second, etc ~ kwanza/ pili. 8 nyumba, nyumbani. 9 (in proper names) mtaa. 10 (football, Rugby) ~ kick kiki ya kuweka mpira chini. 11 (compounds) in ~ katika nafasi yake; (fig) -a kufaa. out of ~ si katika nafasi yake; (fig) -siofaa. in ~ of badala ya. give ~ achia. give ~ to achia nafasi kwa, rithiwa na. make ~ for acha nafasi kwa ajili ya; achia; tanguliwa na. take the ~ of chukua nafasi ya, -wa badala ya. take ~ tukia. pride of ~ nafasi ya juu. placeman, ~-seeker n mtafuta cheo. vt 1 weka (kitu) mahali fulani, panga (kitu) katika nafasi yake. 2 teua (mtu). 3 weka, wekeza. 4 agiza bidhaa. 5 uza/sukuma bidhaa. 6 ~confidence in -wa na imani na. 7 kumbuka/tambua mtu. 8 (racing) shika nafasi. be ~d -wa kati ya washindani watatu wa mwanzo, -wa mshindi.