pass

n 1 kufaulu mtihani. 2 kuwa katika hali fulani; hali. 3 come to/ reach a pretty/sad/strange ~ fikia hali ya ajabu. come to ~ tokea. bring to ~ tekeleza; timiliza. 4 pasi, kibali, pasipoti. 5 (football) pasi. 6 kupitisha mkono juu ya kitu (kama vile wafanyavyo wacheza mazingaombwe). 7 pigo la kwenda mbele (katika mchezo wa kupigana kwa panga).make a ~ at (a woman) (sl) tongoza. 8 (card games) kumruka mchezaji. hold the ~ (fig) tetea hoja. sell the ~ (fig) saliti. 9 njia nyembamba ipitiayo katika milima. 10 (compounds) pass-book n kitabu cha benki; (S Africa) pasi. passkey n ufunguo malaya, ufunguo mkuu. password n neno la siri la kumtambulisha mtu kwa walinzi (agh. katika jeshi). vi,vt 1 pita, nenda. ~ er by mpita njia. 2 acha mtu/kitu nyuma au katika upande fulani na kwenda mbele. 3 ruka, pitia. 4 (of time) tumika, malizika. 5 tumia (muda), pitisha. 6 ~ (from) badilika toka hali moja hadi nyingine. 7 pa, pitisha please ~ me the book tafadhali nipe kitabu hicho. 8 sema, tamka. ~ the time of day with somebody ongea/sogoa na ~ a comment sema kitu. 9 tawanya he was found guilty of ~ing subversive documents alipatikana na hatia ya kutawanya maandishi ya kupotosha umma. 10 pitisha; pita; idhinisha, kubali the Bill ~ed and became law mswada ulipitishwa na kuwa sheria most of the candidates ~ed watahiniwa wengi walishinda. 11 fikia mwisho; kufa; vuka mpaka. 12 fanyika, tendeka, tokea what was ~ing between you two? kulikuwa na nini kati yenu wawili? 13 ~ something on something/somebody hukumu, toa (uamuzi, ushauri n.k.) ~ sentence on an accused man hukumu mshitakiwa. ~ one's word toa ahadi. 14 (card games) ruka (zamu ya mchezaji). 15 (in football, hockey etc) pasia Juma ~ed the ball to Daudi Juma alimpasia Daudi mpira. 16 pita, kuwa nje ya mpaka, zidi. 17 kubaliwa bila lawama; pita bila kuonekana au kusailiwa. 18 enda, fanya kitu kiende au kijongee; pitisha. 19 pitisha majeshi mbele (kwa ajili ya kukaguliwa. 20 (with adv and prep) ~ something/ somebody by pita, puuza, tojali. ~ for kubalika kama/kuwa. ~ off (of events) fanyika, tendeka; acha kujali/ kuangalia; (of pain) isha. ~ something or somebody off as jifanye kuwa. ~ over acha kuzingatia; tojali, acha, sahau. ~ out (colloq) tumia. ~ out (of something) maliza. ~ something on somebody/something toa (uamuzi, ushauri n.k.). ~ in/into chaguliwa. ~ something off kwepa. ~ up puuza. ~ away (euphem) -fa. ~ something on -pa mtu mwingine, pitisha. ~ing out ceremony/parade passe,passee sherehe/gwaride la kumaliza mafunzo. ~ through something -wa na uzoefu, pitia. 21 ~ water kojoa. passable adj 1 -a kupitika. 2 -a kadiri, -a wastani, -a kuridhisha. passably adv. passage n 1 kitendo cha kupita, mpito. a bird of ~age ndege wa kuhama, mpita njia. 2 njia, pito, upenyo. 3 safari. 4 ~age (way) n njia; (nyumbani) ukumbini. 5 yapitayo baina ya watu wawili katika mazungumzo have angry ~ages with somebody wa na mabishano makali. 6 ~ ages of arms n (fig) mapigano; mabishano. 7 dondoo, maneno, fungu la maneno yaliyonukuliwa katika kitabu. 8 kupitishwa kwa mswada kuwa sheria. passing adj -a kupita, -a mara moja n 1 kupita. 2 kifo; kufariki, kufa. ~ing-bell n kengele ya kujulisha kifo/mazishi. in ~ing kwa kupitia tu, wakati wa kusema adv (arch) sana.