1n kiganja, kitanga cha mkono. grease/oil somebody's ~ toa rushwa, honga. have an itching ~ penda kula rushwa/kuhongwa. have somebody in the ~ of one's hand weka mkononi, tawala. vt ficha katika kitanga cha mkono. ~ something off (on somebody) tapeli, toa/pa kwa hila. palmistn mtabiri asomaye kitanga. palmistryn usomaji kitanga.
palm
2n 1 mti wa jamii ya mchikichi n.k. coconut ~ mnazi date ~ mtende. ~ treen mchikichi ~ kernel kiini/nazi/kokwa. ~oiln mawese. ~ winen tembo. P~ Sundayn Jumapili ya Matawi. 2 jani la mnazi (alama ya ushindi). bear/carry off the ~ shinda. yield the ~ to somebody kubali kushindwa (na mwingine). palmyadj -liositawi; -lioneemeka. palmern(formally) hujaji arejeaye kutoka Nchi Takatifu na jani la mnazi.