name
n 1 jina change of ~ kubadili jina full ~ jina kamili list of ~s orodha ya majina assumed ~ lakabu in one's own ~ kwa uwezo wa binafsi, kwa nguvu do something in somebody's ~ fanya kitu kwa jina la fulani. go under the ~ of fahamika kwa jina la know somebody by ~ fahamu mtu kwa jina lake mention no ~s usitaje majina. in the ~ of kwa jina la; kwa ajili ya; kwa amri ya. in the ~ of God haki ya Mungu! kwa jina la Mungu, Bismillahi. call somebody ~s tukana/kashifu mtu. put/enter down one's ~ for jiandikisha, andikisha jina. not have a penny to one's ~ -tokuwa na fedha kabisa. lend one's ~ to ruhusu jina litumike kwa faida ya wengine. take somebody's ~ in vain tumia vibaya/kashifu jina la mtu. ~ day n siku ya sherehe ya somo. ~ dropping n tabia ya kujikombakomba kwa majina ya wakubwa. ~ drop vi tumia majina ya wakubwa kujikomba. ~ part n mshikilia jina la mchezo/mwajina. ~ plate n kibao cha mlangoni. ~ sake n somo. 2 sifa have a bad ~ -wa na sifa mbaya. win a good ~ for oneself/make one's ~ fahamika, jipatia sifa njema. 3 mtu mashuhuri. vt 1 ~ (after/(US) for) -pa jina the boy was ~d after his grandfather kijana alipewa jina la babu yake. 2 taja ~ what you want taja unachotaka. 3 ~ (for) teua. ~ for an office -pa cheo. 4 ainisha ~ all animals in Serengeti ainisha/taja majina ya wanyama wote katika Serengeti. 5 toa bei ~ your price sema uwezo wako, utatoa ngapi. nameless adj 1 bila jina. 2 -siofaa kutajwa (kwa kuwa -baya mno). 3 -sioelezeka.