meat

n 1 nyama; (without bones) mnofu, chinyango; (with rice etc) kitoweo lean ~ mnofu (bila shahamu); (US of fruits, nuts, shellfish) nyama. 2 (arch) chakula, mlo. one man's ~ is another man's poison halali yako ni haramu ya mwingine. ~ and drink kipenzi, -enye kupendwa sana football is his ~ and drink mpira wa miguu ni mchezo anaopenda sana, ndio ulevi wake. 3 (fig) uzito, mambo ya maana this short article contains a lot of ~ makala hii ndogo ina mambo ya maana. 4 (combined forms) meatball n kababu. ~ chopper n kishoka. ~ grinder n kisagio nyama ~loaf bofulo ya nyama. ~-safe n kabati ya nyama, chakula. (GB) ~ tea n chai kuu (jioni); chai pamoja na nyama. meatless adj bila nyama. meaty adj (fig) -enye maana, muhimu.