measure

n 1 kipimo; kimo. take somebody's ~ (fig) pima/angalia tabia, akili, uwezo n.k. wa mtu. give full/short ~ toa kiasi kamili/ pungufu give extra ~ toa nyongeza. made to ~ (of clothes) iliyopimwa ~ of spread kipimo cha mweneo. 2 kiasi, kiwango. in some ~ kwa kiasi fulani. beyond ~ kupita kiasi. without ~ bila kiasi. 3 (music, poetry) mapigo, mwendo. tread a ~ with somebody cheza dansi na. 4 chenezo, kipimo, kigezo. greatest common ~ n (abbr GCM) namba kubwa kabisa inayogawa namba nyingi zote sawasawa/bila kuacha mabaki. 5 hatua, mashauri, matendo take ~s to rectify the situation chukua hatua za kurekebisha hali. set ~s to wekea mipaka. 6 sheria (iliyopendekezwa). vt,vi 1 pima (ukubwa/kiasi n.k.). 2 tathmini. ~ somebody angalia tabia ya mtu. 3 ~ up to the job -wa na uwezo wa kufanya kazi. ~ one's length anguka kifudifudi. ~ swords against/with somebody (fig) pimana nguvu na. ~ one's strength (with somebody) jaribu nguvu/uwezo. 4 fikia, -wa na (urefu wa n.k.). it ~s six feet urefu wake ni futi sita. 5 ~ out/off toa kidogo kidogo; pambanua. measured adj -a taratibu; -a sawasawa; (of language) -liofikiriwa, zito. measurable adj -a kupimika. measureless adj bila kikomo, -sio na mipaka. measurement n 1 kipimo. inside ~ment n vipimo vya ndani; (transportation) bidhaa zinazogharimiwa kwa kipimo badala ya uzito. 2 (pl) vipimo (vya marefu, mapana na kina).