love

n 1 upendo, mapenzi, huba a mother's ~ for her children mapenzi ya mama kwa watoto wake. give/ send somebody one's ~ tuma salamu (zenye upendo). play for ~ cheza kwa kujifurahisha tu. not to be had for ~ or money -sioweza kupatikana (kwa njia yoyote). there is no ~ lost between them hawapendani. a labour of ~ kitu mtu anachofurahia kufanya; kumfanyia mtu kitu kwa sababu ya upendo. for the ~ of (in appeals etc) kwa jina la..... ~feast n (rel) karamu ya pamoja (iliyoadhi- mishwa na Wakristo wa zamani kudumisha upendo); ibada ya pamoja. 2 mapenzi, mahaba. be in ~ (with love somebody) penda mwanamke/ mwanamme John is in ~ with Mary, John anampenda Mary. fall in ~ (with somebody) penda mwanamke/mwanamume. make ~ (to somebody) lala; jamiiana, fanya mapenzi; onyesha kupendana na. 3 (compounds) ~ affair n uhusiano wa kimapenzi. ~ bird n kasuku mdogo; (pl) watu waliopendana sana. ~-child n mwanaharamu. love-knot n fundo mapenzi. ~-letter n barua ya mapenzi. love-lorn adj -a simanzi (agh. kwa kumkosa mpenzi); -a kunyong'onyea (agh. kutokana na mapenzi). love-making n kujamiiana (na mambo yote yanayohusiana na kitendo hicho). ~-match n ndoa itokanayo na mapenzi tu. ~-philtre/-potion n dawa ya mapenzi. ~-seat n benchi mfano wa S yenye sehemu mbili za kukalia zilizopeana migongo. love-sick adj -a simanzi, nyong'onyevu (kwa sababu ya mapenzi). lovesickness n ugonjwa wa mahaba. ~-song n wimbo wa mapenzi. ~-story n hadithi ya mapenzi/huba. ~-token n hidaya. 4 (colloq) mpenzi, kipenzi (agh. mke, mme, au mtoto) come here my ~ njoo hapa kipenzi changu. 5 mpenzi. 6 (in games) bila, bure. ~ all bila bila; hakuna bao pande zote. loveless adj -siopenda; -siopendwa; pasipo penzi. vt 1 penda ~ one's parents penda wazazi. 2 abudu. 3 (colloq) penda sana; furahia. lovable adj -a kupendeka. lovely adj 1 -zuri sana, -a kupendeza; -a kufurahisha. 2 (colloq) safi, -a kuchangamsha, -a kuburudisha what a ~ly meal! chakula safi sana. loveliness n. lover n 1 mpenzi they are ~rs ni wapenzi. 2 (of music, football etc.) mpenzi, shabiki. ~like adj -enye mapenzi. loving adj -enye upendo. ~-cup n bilauri/kata ya pombe (ambayo huzungushwa kwa zamu kutoka mnywaji mmoja hadi mwingine). ~-kindness n wema, huruma, (of God) rehema. lovingly adv.