look
vi,vt 1 ~ (at) tazama, angalia. to ~ at him/it etc. (in passing judgement) ukimwangalia kwa nje. L~ before you leap (prov) tahadhari kabla ya kufanya jambo. ~ing glass n kioo (cha kujitazamia). ~ somebody/something in the eye(s)/face angalia mtu usoni; kabili. 2 onekana ~ ill onekana mgonjwa ~ oneself onekana kama kawaida ya mtu alivyo. ~one's age lingania/oana na umri wake you don't ~ your age huonekani kuwa mzee kiasi hicho. ~ one's best pendeza she ~s her best in skirts anapendeza akivaa sketi. ~ black (at) angalia kwa hasira. ~ blue sononeka; nuna. ~ good pendeza vutia; onekana kuwa na maendeleo mazuri. good looking adj -enye sura/umbo la kupendeza. ~ small onekana duni. L~ alive! Changamka! L~ here! Sikiliza! Angalia! L~ sharp! Changamka! Fanya haraka! ~ well (of persons) onekana mwenye afya njema; (of things) onekana -a kupendeza, vutia; (of a person wearing something) pendeza. 3 ~ like/as if onekana kama, elekea it ~s like we will win inaelekea tutashinda. 4 angalia ~ where you are going angalia unakokwenda! 5 onyesha (kwa sura). 6 (uses with adverbial particles and preps) ~ about (for something) tafuta; angalia kwa makini, chunguza. ~ about one fanya uchunguzi ~ after somebody/something tunza; sindikiza kwa macho. ~ at something (special uses) not ~ at something (usu with will, would) -toangalia, -tofikiria; -tochunguza; (in polite requests) angalia. good/bad etc. to ~ at -enye sura ya kupendeza/kuchukiza n.k,. onekana vizuri, vibaya n.k. ~ away (from something) kwepesha macho. ~ back (on/to something) (fig) tazama nyuma, kumbuka ya nyuma. never ~ back usirudi/tazame nyuma; endelea (bila kukatishwa). ~ down on somebody/something (colloq) angalia kwa dharau/chuki. ~ for somebody/something tafuta; tarajia it is too early to ~ for results ni mapema mno kutarajia matokeo. ~ forward to something ngojea kwa hamu/shauku. ~ in (on somebody) tembelea (mtu) kwa muda mfupi. give somebody/get a ~-in (colloq, sport, etc.) toa/pata nafasi, fursa (ya kushinda n.k.) you won't get a ~- in with such strong competition hutapata fursa ya kushinda/huwezi kushinda katika ushindani mkali namna hiyo. ~ into something chunguza; peleleza; soma kwa kupitia (kitabu n.k.); angalia ndani ya kitu. ~ on -wa mtazamaji, tazama, looker on n mtazamaji. ~ on/upon somebody/something as ona kama do you ~ on him as an authority on biology? unamwona kama bingwa wa biolojia? ~ on/upon somebody something with ona mtu/jambo kuwa ni he seems to ~ on me with distrust anaelekea kutoniamini. ~ on to elekea the hotel room ~s on to the beach chumba cha hoteli kinaelekea ufukoni. ~ out (of something) (at something) tazama. ~ out on (to)/over elekea. ~ out (for somebody/something) jihadhari, -wa macho -wa tayari kwa. L~ out! Tahadhari! ~-out n keep a good ~-out (for); be on the ~-out (for) -wa mwangalifu, -wa macho; (mil) mahali pa kulindia, ulingo; mlinzi (sing only) (prospect) jambo la kutarajiwa, matarajio that's your own ~ out! shauri yako! ~ something out for somebody chagulia mtu kitu (baada ya kukichunguza). ~ over something kagua, chunguza. ~ something over kagua sehemu mojamoja. look-over n ukaguzi. ~ round (fig) angalia uwezekano (kabla ya kufanya jambo); geuza kichwa (kuangalia kila upande). ~ round (something) tembelea/zungukia mahali, (ili kuangalia). ~ through something durusu. ~ something through kagua kitu kwa makini. ~ to something chunga, angalia. ~ to somebody for something/to do something tegemea mtu kwa jambo/ kwa ajili ya kufanya jambo. ~ to/towards elekea. ~ up angalia juu; tengemaa, ongezeka bei au ufanisi. ~ something up tafuta kitu kitabuni n.k. ~ somebody up tembelea mtu. ~ somebody up and down kagua mtu; tazama (mtu) kwa dharau. n 1 mtazamo, kutazama let me have a ~ at your leg hebu nitazame mguu wako. 2 sura, kuonekana. give something/get a new ~ -pa/pewa sura mpya. 3 (pl) sura (ya mtu). looker n a good ~er mtu mwenye sura nzuri.