live
live
1 adj 1 -hai, -enye uhai ~ weight uzito wa mnyama hai. 2 -a moto; motomoto; -a kuwaka; (of issues) motomoto, -a kisasa, sasa hivi ~ coals makaa ya moto; (of bullets, bombs) -enye marisawa; (elect) -enye umeme. ~ wire n waya moto/wenye umeme; (fig) (persons) mchangamfu. 3 (radio/TV) a ~ broadcast tangazo la moja kwa moja (lisilorekodiwa kabla). 4 ~ -birth n mtoto aliyezaliwa hai. 5 -a nishati; mashughuli; -a hima.live
2 vt,vt 1 ishi, -wa na uzima, -wa hai. 2 endelea kuishi, dumu. ~ on jikongoja, endelea kuishi. you/we ~ and learn kuishi kwingi kuona mengi. ~ and let ~ -wa mvumilivu long ~ somebody! adumu fulani maisha marefu! ~ honestly -ishi kwa uaminifu ~ to be.... ishi hadi... ~ through, shinda majaribio mengi, vumilia ~ as man and wife kaa kinyumba. ~ to oneself jitenga, ishi pekee. 3 pata riziki. ~ by tegemea. what does he ~ by kazi yake nini? ~ by one's wits ishi kwa ujanja/mbinu. ~ off the land tegemea riziki kwa kilimo. ~ on something ishi kwa kutegemea kitu. ~ on your salary ishi kwa kutegemea mshahara wako what does he ~ on? anaponea nini? ~ on one's name/reputation ishi kwa sifa/jina zuri. 4 ~(in/at) (reside) ishi, -kaa; (of room etc) not fit to ~in haifai kuishi ndani yake, haikaliki. 5 ~ on (in memory etc) dumu, ishi katika kumbukumbu ya watu. ~ together ishi pamoja. ~ in/out (of domestic servants) ishi kazini/ nyumbani, nenda na kurudi kila siku. 6 nenda. ~ up to something fuata; fikia matarajio fulani. ~ something down sahaulisha yaliyopita. ~ with something vumilia. 7 ~ it up ishi maisha ya mishughuliko na anasa, furahia maisha. 8 ishi uonavyo; chagua kuwa mwaminifu. ~ a lie ishi kinafiki. livable; ~able adj 1 -a kukalika; -enye kufaa kuishi. 2 -a kuvumilika. livelihood n kazi, riziki. earn a ~lihood chuma riziki. livelong adj (only in) the ~long day mchana kutwa. the ~long night usiku kucha adj 1 -epesi; changamfu, -cheshi, -kunjufu. 2 (of non-living things) -a kwenda mbio have a ~ly time sisimkwa, changamka. look ~ly changamka. make things ~ly for somebody changamsha, sisimua mtu. 3 (of colour) kali, -enye kung'aa. 4 hai, kama kweli/halisi. liveliness n. liven vt,vi ~ up changamsha, sisimua; sisimka. liver n mtu apendaye kuishi kwa namna yake (nzuri au mbaya).