life

n 1 uhai. ~ force n nishati uhai. 2 viumbe/vitu hai (watu, wanyama na mimea). 3 maisha. a matter of ~ and death struggle mapambano ya kufa na kupona ~ insurance bima ya maisha. bring to ~ huisha. come to ~ pata fahamu baada ya kuzimia; changamka. run for ones ~/for dear ~ kimbia ili kujiokoa/kunusuru maisha. this ~ maisha ya hapa duniani. the other ~; future/ eternal/everlasting ~ n maisha ya peponi; ahera. with all the pleasure in ~ kwa raha mustarehe. 4 take somebody's ~ ua mtu. take one's own ~ jiua, jinyonga. a ~ for a ~ mtu kwa mtu, kulipiza kisasi. can not for the ~ of one haiwezekani hata kama mtu akijitahidi kiasi gani. not on your ~! (colloq) la hasha! thubutu. 5 kipindi katika maisha (k.m. kuzaliwa hadi kufa) he lived here all his ~ aliishi hapa maisha yake yote the ~ of the government maisha ya serikali ilipokuwa inafanya kazi he was given a ~ sentence alipata kifungo cha maisha. ~ annuity n fedha alipwazo mtu mpaka atakapokufa for ~ kabisa, kwa maisha. ~ cycle n hatua anuwai za maisha kamili ya kiumbe (k.m. mbu kuanzia yai, kiluwiluwi, pupa hadi mdudu kamili). ~ interest n (legal) mapato (kutokana na mali fulani) apewayo mtu wakati wa uhai wake tu. ~ peer n mjumbe wa baraza la malodi (Uingereza) ambaye cheo chake hakirithiki. have the time of one's ~ (colloq) jistarehesha sana. early/late in ~ mapema, mwanzoni/mwishoni mwa maisha. 6 uhusiano, uchangamfu, starehe there is little ~ in the villages vijijini hakuna shughuli nyingi/hapakuchangamka; maisha yamedorora vijijini the children are full of ~ watoto wamechangamka/ wana raha. true to ~ (of a story, drama etc.) -enye kutoa picha halisi ya maisha; (of interest/way of living) -a kupendeza, -a kuvutia put more ~ in your work fanya kazi yako ivutie, changamkia kazi zaidi. the ~ (and soul) of the party mtu aliye mchangamfu sana katika kikundi. 7 wasifu a ~ story of Julius Nyerere wasifu wa Julius Nyerere. 8 mfano/ kielezo chenye uhai a ~ drawing picha iliyochorwa kwa kutumia mfano wa kiumbe hai, vitu hai. to the ~ kwa usahihi. as large as ~ -enye ukubwa wa kawaida (colloq and in joke) -enyewe, binafsi; kwa uhakika; pasipo shaka yoyote. 9 maisha baada ya kunusurika. 10 (compounds) ~belt n mkanda wa kujiokolea. life-blood n kiini; damu muhimu kwa uhai; (fig) jambo lenye athari kubwa; kitu kinachotia nguvu. ~-boat n mashuaokozi (ya kuokolea watu au inayochukuliwa melini). lifebuoy n boyaokozi (chelezo cha kuopolea/kuokolea watu katika hatari ya majini). ~ estate n milki ya maisha (ambayo mtu hutumia hadi anapokufa na hairithishwi). ~ expectancy n miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi. life-giving adj -a kuhuisha. ~-guards n walinzi, waokozi katika sehemu za kuogelea. L~ Guards n (pl) kikosi cha farasi katika jeshi la Kiingereza. ~ history n (biol) kumbukumbu ya maisha kamili ya kiumbe. ~ insurance/ assurance n bima ya maisha. ~-jacket n jaketi/koti okozi. lifelike adj -enye kufanana na kiumbe chenye uhai; -enye kufanana na kiwakilishwa. lifeline n 1 kambaokozi: kamba ya kuokolea maisha (ambayo hufungwa kwenye boya au meli); kamba ya wapiga mbizi; (fig) tegemeo kuu; kitu kinachotegemewa kwa uhai wa mtu. lifelong adj -a maisha, -a maishani. ~-office n ofisi ya bima ya maisha. life-preserver n (US) ~ jacket n (GB) rungu la kujilinda. life-saver n (colloq) kitu/mtu amsaidiaye mwenzake katika matatizo (esp in Australia); mwogeleaji aokoaye watu waliozama. ~-sentence n adhabu ya kifungo cha maisha. ~-size(d) adj (picha) -enye ukubwa sawa na kitu chenyewe. ~-span n (biol) maisha ya kiumbe/kitu. ~-support system n vifaa kwenye chombo cha anga/ hospitali ambavyo humsaidia mtu kuishi. lifetime n maisha. the chance of a ~ time bahati inayotokea mara moja katika maisha. in somebody's ~ time katika maisha ya mtu. ~-work n kazi ya kudumu, kazi yenye kumshughulisha mtu maisha yake yote. lifeless adj -fu, -liokufa; -siokuwa na uhai; -enye kuchusha, -siovutia. lifelessly adv. lifer n (sl) mtu aishiye kwa namna fulani (sl) mfungwa wa maisha.