lie
lie
1 vi danganya, sema uwongo she is lying anadanganya. n uwongo tell a ~sema uwongo. give somebody the ~ shitaki mtu kwa kudanganya. ~ detector n kijaluba cha kupimia mabadiliko kifiziolojia (k.m. mapigo ya moyo, kupumua hasa wakati mtu anapohojiwa); kibaini uongo.lie
2 vi 1 lala, jinyoosha juu ya kitanda, ardhi n.k. ~ on one's back lala chali ~ back jinyoosha ~ face downwards lala kifudifudi her body ~s at the cemetery amezikwa makaburini. take something lying down kubali kutukanwa pasi na ubishi. ~ down under (an insult) kubali bila kupinga. ~ in kawia kuamka (kutoka kitandani); -wa katika uchungu kitandani (ili kuzaa mtoto). lying -in hospital (old use) hospitali ya uzazi. ~ up lala kitandani au chumbani kwa ugonjwa. ~ with (old use biblical, now usu sleep with) jamiiana. let sleeping dogs ~ (prov) usimwamshe aliyelala, ukimwamsha utalala wewe. ~-a bed n mvivu, asiyetaka kuamka kitandani. 2 (of things) -wa juu ya the coat lay on the floor the whole night koti lilikuwa juu ya sakafu usiku kucha. 3 (of abstract things) -wa, -wa katika hali fulani I know where his interest ~s nafahamu mambo anayoyapendelea the car's trouble ~s in the gear box tatizo la gari limo ndani ya gia boksi. ~ at somebody's door husika, laumika at whose door should the defeat ~? nani alaumiwe kwa kushindwa kwetu? ~ with somebody wajibika it ~s with you to appoint your deputy unawajibika kumteua naibu wako. as far as in me ~s kwa kadri ya uwezo wangu. 4 -wa mahali. ~ to (of a ship) karibia kusimama, kabili upepo. 5 kaa, baki the youth are lying around idle in town vijana wanakaa bure mjini the soldier lay in the cell for one more night askari alikaa rumande kwa usiku mmoja zaidi. ~ heavy on something lemea, dhuru. ~ over ahirishwa kwa jambo. 6 enea, zagaa, tanda the game lay before us wanyama walizagaa kila mahali mbele yetu. find out/see how the land ~s (fig) jifunze, chunguza, dadisi jinsi hali ya mambo ilivyo. 7 (legal) kubalika his appeal will not ~in the court of law rufaa yake haitakubaliwa na mahakama. n (sing only) mkao/mlalo wa kitu. the ~ of the land jinsi sura ya nchi ilivyo (fig) hali ya mambo.