length

n 1 urefu be 5 miles in ~ -wa na urefu wa maili tano; (period of time) muda wa the ~ of our stay was two days tulikaa kwa muda wa siku mbili. at ~ mwishowe; hatimaye; kwa muda mrefu; kwa undani. (at) full ~ lala kwa kujinyoosha. keep somebody at arms ~ kataa urafiki na mtu, epa. 2 kadiri, kiasi. go to any ~ (s) fanya kila linalowezekana (kupata utakacho). 3 kipande cha (nguo, bomba n.k. kinachotosha shughuli fulani) I need a ~ of dress material ninahitaji kipande cha kitambaa cha gauni. 4 kipimo cha kitu mwanzo hadi mwisho; urefu. lengthen vt,vi refusha. lengthways; lengthwise adv, adj kwa urefu. lengthy adj -refu mno.