leave

vt,vi 1 toka, ondoka; we shall~ here tomorrow tutaondoka hapa kesho. ~ for ondoka kwenda/ kuelekea (mahali fulani) ~ for Nairobi ondoka kwenda Nairobi. 2 (of a thing, person, work, place) acha ~ your books here acha vitabu vyako hapa ~ a guest at home acha mgeni nyumbani she expects to ~ the job anatarajia kuacha kazi when did you ~ school? ulimaliza shule lini? be/get nicely left (colloq) danganywa; telekezwa. ~ somebody/something behind sahau, acha don't ~ me behind usiniache. ~ somebody/something alone -tosumbua, -toingilia, -togusa. ~ well alone (prov) usitie ufundi kwenye kitu kizuri, acha mambo yalivyo. ~ off acha; koma, isha, hulu where did we ~ off? tulikomea/tuliachia wapi when did you ~ off your spectacles? lini umeacha kuvaa miwani yako? ~ something/somebody out ruka, acha (kumshughulikia). ~ something over ahirisha, acha (kwa muda). ~ it at that achia hapo, acha kusema/ kufanya zaidi. ~ somebody to himself/to his own devices acha huru. ~ something unsaid acha kusema jambo. ~ much/a lot/ something/to be desired -toridhisha. ~ nothing to be desired ridhisha. ~ go/hold (of something) achilia. 3 baki, bakisha ~ some money for clothes bakisha kiasi cha fedha kwa ajili ya nguo eight from ten ~s two kumi ukitoa nane hubaki mbili. to be left until called for ikae/iachwe hadi mwenyewe aje kuchukua. 4 -pa, achia; kabidhi. ~ word (with somebody) (for somebody) -pa/ achia maagizo n.k. ~ the matter to somebody achia mtu shauri alishughulikie ~ a teacher on duty in charge of the school achia/kabidhi madaraka ya shule kwa mwalimu wa zamu. 5 ~ something (to somebody); ~ somebody something (at the time of one's death) rithisha, acha/achia (mali, madeni, mjane, watoto n.k.). 6 (of directions) pita ~ the post office on your right pita posta upande wa kulia. n 1 ruhusa, idhini. ~ of leaven absence likizo/ruhusa (ya kutokuwepo) ~ to appeal ruhusa ya kukata rufaa. by/with your ~ kwa ruhusa yako, kumradhi. 2 likizo, livu emergency ~ likizo ya dharura sick ~ likizo ya ugonjwa. take French ~ toroka, enda likizo bila ruhusa. on ~ likizoni. 3 kuondoka. take (one's) ~ (of somebody) aga, agana na. ~ taking n kuaga/kuagana. take ~ of one's senses fanya kama mwenda wazimu; pata wazimu. leavings n (pl) mabaki, masalio, masazo, makombo.