lay

lay

1 n (chiefly in) the ~ of the land sura ya nchi.

lay

2 adj 1 (RC) -a mtu wa kawaida, -a mlei ~ brother bruda mfanyakazi. 2 -sio -eledi ~ opinion mawazo ya watu wa kawaida. layman n (mtu) mlei, asiye mtaalam.

lay

3 n (lit) wimbo; utenzi.

lay

4 n mwenzi katika kujamiiana/ kukazana.

lay

5 vt,vi 1 weka, laza; tandaza he laid his hand on my shoulder aliweka mkono wake begani mwangu. ~ a snare/trap/an ambush (for somebody/something) tega mtego/tegea mtu, tayarisha mtego/uvamizi. 2 (of non-material things, and fig uses) weka. ~ (one's) hands on something/somebody) nyang'anya; chukua he keeps everything he can ~ his hands on huchukua kila kitu anachokiona; umiza, jeruhi; pata; (eccles) bariki. ~ing-on of hands uwekaji wakfu; kufanya kasisi; uthibitisho. ~ the blame for something on somebody laumu, twisha/tupia lawama. ~ a (heavy) burden on somebody pa kazi/wajibu mzito; pa mateso. ~ one's hopes on wekea matumaini. ~ a strict injunction on somebody (to do something to) amuru. ~ great/ little store by/on something, thamini sana/kidogo. ~stress/emphasis/ weight on something fanya kuwa muhimu, sisitiza. ~ a tax on something toza kodi. 3 sababisha hali fulani. ~ somebody to rest zika. ~ somebody under a/the necessity/ obligation lazimisha, shurutisha. ~ somebody under contribution lazimisha mtu atoe mchango. ~ something to somebody's charge -pa wajibu. 4 (~+n, adj or adv phrases) ~ something bare onyesha kwa uwazi kabisa, fichua. ~ something flat sambaza, tandaza. ~ something open fichua, onyesha waziwazi, funua, eleza; kata. ~ oneself open to something jiweka katika hali ya kulaumiwa, kushukiwa n.k. ~ something waste angamiza, teketeza. 5 tuliza. ~ somebody's doubts ondosha mashaka. ~ a ghost/spirit fukuza/punga mizimu/mashetani. 6 (of birds and insects) taga mayai. 7 (usu passive) (story) tokea (katika mahali fulani). 8 tayarisha, andaa, panga ~ the table andaa meza ~ the fire tayarisha moto mekoni. 9 weka dau. 10 tandika, funika ~ carpet on the floor tandika zulia sakafuni. 11 (sl) jamiiana; kaza, tia. 12 (use with adverbial particles and preps) ~ about one (with something) pigapiga, piga pande zote. ~ something aside weka akiba; weka chini, acha (tabia fulani n.k.). ~ something back laza geuza/geuka, pindua/pinduka. ~ something by weka akiba. ~ somebody/oneself down laza/jilaza. ~ something down lipa; anza kujenga meli n.k.; geuza shamba kuwa sehemu ya malisho; hifadhi (divai) ghalani (agh. chini ya ardhi). ~ something down; ~ it down that agiza, panga (kanuni, sheria, utaratibu n.k.). ~ down one's arms weka silaha chini (kama ishara ya kusalimu amri). ~ down the law amuru. ~ down one's life jitolea mhanga. ~ down office jiuzulu. ~ something in weka akiba ya. ~ off (colloq) acha kufanya kazi; pumzika; acha kufanya jambo la kuudhi. ~ somebody off achisha kazi kwa muda. ~ off n muda ambao watu wanakuwa wameachishwa kazi. ~ something on weka gesi, maji, umeme kwenye jengo; colloq) toa, panga. ~ it on (thick/with a trowel) visha kilemba cha ukoka. ~ something out tanda, tandaza; osha/tayarisha (maiti) kwa kuzika; (colloq) tumia fedha; panga. layout n mpango; mpangilio wa (kurasa, tangazo, kitabu n.k.), utaratibu. vt ~ out one's money carefully tumia fedha kwa uangalifu; weka mipango/utaratibu wa kazi, panga. ~ oneself out (to do something) jitahidi; jiandaa. ~ over (US) (GB stop over) (journey) simama kwa mapumziko. layover n mapumziko ya safarini. ~ something up weka akiba; jichimbia kaburi you're ~ing up trouble for yourself in the future unajichimbia kaburi; simamisha shughuli za meli kwa ajili ya matengenezo. ~ somebody up (usu passive) sababisha (mtu abaki kitandani).

lay

6 pt of lie2