land

n 1 ardhi, nchi kavu travel over ~ safiri nchi kavu go by ~ enda kwa gari, treni n.k. 2 shamba, konde; kiwanja work on the ~ fanya kazi shambani. ~army n (GB) kikosi cha wafanyakazi wa kike wa shamba wakati wa vita vikuu vya pili Our ~ is about ten hectares shamba letu lina ukubwa wa hekta kumi. ~ agent n (chiefly GB) (US real estate agent) mwangalizi/msimazi wa shamba; wakala wa mashamba/viwanja. 3 nchi, taifa (la asili ya mtu) my native ~ nchi yangu ya asili distant ~s nchi za mbali. the ~ of the living maisha ya sasa I'm still in the ~ of the living bado nipo the promised~/ the ~ of Promise Nchi ya Ahadi (Canaan). 4 (compounds) ~ fall n kukaribia nchi kavu (kutoka majini). ~ forces n jeshi la nchi kavu. ~ holder n mmilikaji wa ardhi. ~ lady n mwanamke mwenye hoteli/nyumba ya kupangisha. ~ locked adj -liozungukwa na nchi kavu ~ locked countries nchi zisizokuwa na bandari. ~ lord n kabaila; mwenye hoteli/nyumba ya kupangisha. ~ lubber n (used by sailor) (mtu) asiye baharia. landmark n alama (k.m. mnara, n.k.); alama ya mpaka; (fig) jambo/tukio/wazo muhimu (linalodhihirisha) upeo au mabadiliko. ~ mine n mabomu ya ardhini. ~ owner n mmiliki ardhi. ~ rover n landrova: gari madhubuti la barabara mbaya. ~ slide n mporomoko wa ardhi; (in election) ushindi mkubwa ~slide victory ushindi mkubwa sana. ~ slip/slide n. ~s man n mtu asiye baharia. vt,vi 1 (of aircraft) tua; (of ship) fika pwani, teremka pwani the aeroplane ~ed at night ndege ilitua usiku the passangers ~ed when the ship anchored at the harbour abiria waliteremka (pwani) meli ilipotia nanga bandarini. ~ on one's feet (fig) -wa na bahati; nusurika. 2 ~ somebody/oneself in something ingia matatani. ~ up (colloq) wasili; jikuta, ishia because of his bad behavior one day he ~ed up in jail kutokana na tabia yake mbaya siku moja alijikuta jela Juma ~ed up this morning unexpectedly Juma aliwasili asubuhi hii bila kutegemewa. 3 (colloq) pata ~ a good job pata kazi nzuri. 4 (sl) piga/ chapa (kibao/ngumi) he ~ed him one... alimpiga kibao kimoja ... landed adj -a ardhi; -enye kumiliki ardhi/shamba. landless adj -siokuwa na ardhi/shamba. landing n 1 kushuka/ kutua/ kuteremka pwani (nchi kavu). ~ craft n meli ya kushushia pwani/ufukoni (magari ya kivita, askari n.k.). ~ field/strip n kiwanja cha kutua ndege. ~ gear n marandio. ~ net n fuko la kutilia/kuzolea samaki. 2 (also ~ place n) gati, bunta. ~ party n kikosi cha askari (agh. wa kutuliza fujo). ~ stage n kikwezo. 3 jukwaa la ngazi.