just

just

1 adj 1 -a haki, nyofu, -adilifu a ~ sentence hukumu ya haki a ~ person (mtu) mwadilifu. 2 (well-deserved) -enye kustahiki; -liostahili. justification n 1 kitu au sababu zinazothibitisha. 2 kuthibitisha jambo kuwa ni haki, kusadikisha. 3 haki, halali without ~ification bila ya haki/ uthibitisho. in ~ification (for/of something/somebody) kwa kuthibitisha/ kutetea jambo. justify vt 1 tetea, thibitisha uhalali wa jambo/ tendo ~ify the punishment you meted out thibitisha uhalali wa adhabu uliyoitoa. 2 -wa na sababu ya kufanya jambo, halalisha finishing your work early does not ~ify your loitering kumaliza kazi kwako mapema sio sababu ya kukufanya uzurure. 3 (of print) rekebisha. justifiable adj. ~ ifiably adv.

just

2 adv 1 used (GB) in the perfect tenses and (US often) with the simple past tense placed with the v to indicate an immediate past (GB) sasa hivi, ndio kwanza I have ~ finished my work ndio kwanza nimemaliza kazi yangu. ~ now sasa hivi. 2 (followed by n phrases and clauses) hasa this is ~ the person I wanted to see huyu ndiye hasa mtu niliyetaka kumwona. 3 ~ as (+adj+as) sawasawa na it is ~ as good as mine ni kizuri sawasawa na changu (introducing adverbials of time) wakati he brought it ~ as you were leaving alikileta wakati ule ule ulipokuwa unaondoka (introducing clauses of comparison) jinsi ~ as you find it difficult to depend on your pay jinsi inavyokuwia vigumu kutegemea mshahara wako. 4 (with adv) ~ here hapa hapa. 5 (used to indicate approximation) takribani it was ~ about 9.00 a.m. Ilikuwa takribani saa 3.00 asubuhi tu. 6 (only) He ~ managed to get the fare amefanikiwa kupata nauli tu I have ~ enough money for food nina fedha za kununulia chakula tu I am ~ an ordinary person mimi ni mtu wa kawaida tu. 7 (used in familiar colloqual style) hebu ~ look at this and see how good it is hebu tazama hiki na uone jinsi kilivyo kizuri. 8 (colloq) sana, mno the story was ~ too good hadithi ilikuwa nzuri mno. 9 wakati huuhuu/uleule. ~ now muda huu; muda kitambo, punde Saida left ~ now Saida ameondoka punde.