house

n 1 nyumba. get on like a ~ on fire (of people) elewana haraka sana, fanya urafiki baada ya muda mfupi wa kufahamiana. under ~ arrest kuzuiliwa nyumbani. 2 (usu with a pref) kibanda, jengo, nyumba hen ~ kibanda cha kuku store~ ghala. warehouse n bohari. custom house jengo la ushuru. the H~ of God n Nyumba ya Mungu, kanisa. ~ of cards n nyumba ya karata; (fig) mpango wa wasiwasi. ~ of ill fame (old use) danguro. on the ~ kwa gharama ya kilabu au kampuni. 3 bunge enter the H~ chaguliwa kuwa mbunge. 4 keep a good ~ fadhili/kimu nyumba vyema. keep open ~ -wa tayari kupokea wageni nyumbani wakati wowote, -wa mkarimu. set/put one's ~ in order nyoosha mambo yako. 5 ukoo, jamaa agh. ya watawala. 6 (theatre) hadhira. bring down the ~/bring the ~ down shangiliwa sana na wote waliopo. 7 (compounds) ~ agent n wakala wa nyumba. houseboat n mashua nyumba, mastakimu. housebound adj -liozuiliwa nyumbani. ~ breaker (US housewrecker) n jambazi (avunjaye nyumba ili aibe); mtu anayeajiriwa kubomoa majumba. housecoat n koti la nyumbani. housecraft n maarifa ya utunzaji wa nyumba. ~dog n mbwa mlinzi/anayelinda nyumba. ~ father/mother n mlezi wa makazi ya watoto. ~ flag n bendera ya shirika la meli. housefly n nzi. houseful n nyumba iliyojaa (watu). household n kaya. ~hold guards n watumishi/ wanajeshi wa mfalme. household word n neno/jina litumikalo na wengi. householder n mwenyeji, mwenye nyumba. housekeeper n msimamizi/ mtunzaji wa nyumba. houselights n taa za sinema (n.k.). housemaid n mhudumu wa nyumbani. ~ maid's knee n uvimbe wa goti. houseman n (GB) daktari msaidizi wa mtaalam akaaye hospitali. housemaster n mwalimu mlezi wa bweni. ~ party n wageni wa siku kadhaa shambani. ~ physician n daktari akaaye hospitali. ~proud adj -enye fahari kubwa ya kutunza nyumba. houseroom n nafasi. ~sparrow n shorewanda. ~ surgeon n daktari mpasuaji akaaye hospitali. ~ top n (chiefly in) cry/publish/proclaim something from the ~tops tangaza hadharani. ~ trained adj (of domestic pets) -liofunzwa, -liofundishwa kuwa safi katika nyumba. ~ warming n sherehe ya kuhamia nyumba mpya. housewife n mke afanyaye kazi za nyumbani. ~ wifely adj -a kuhusu mke afanyaye kazi za nyumbani. housewifery n kazi za mke wa nyumbani. housework n kazi za nyumbani. vt 1 -pa nyumba, karibisha. 2 weka/hifadhi vitu (agh. vyombo na vitabu) n makazi. housing association shirika la kujenga na kugawa nyumba (bila kupata faida). housing estate eneo la nyumba za kupanga au kuuz(w)a.