horse

n 1 farasi. a dark ~ n mtu ambaye bahati/nyota yake haijajulikana. a ~ of another colour jambo tofauti kabisa. back the wrong ~ unga mkono mshinde katika shindano. be/get on one's high ~ dai/kazania kupewa heshima inayostahili. eat/work like a ~ -la sana/fanya kazi kwa bidii. hold one's ~ taradadi, sita. look a gift ~ in the mouth pokea kitu bila shukrani. (straight) from the ~'s mouth (of tips, advice, information) halisi, toka kwa mwenyewe/ mhusika. 2 (collective sing) askari wapanda farasi ~ and foot askari wapanda farasi na wa miguu. ~ artillery n mizinga inayovutwa na farasi. 3 kiango, kitegemezi, farasi a clothes ~ kiango cha kuanikia nguo a towel ~ kiango cha kutundikia taulo. 4 (compounds) horseback n. (only in) on ~back mgongoni mwa farasi. horsebox n gari la kubebea farasi. ~ breaker n mfunga farasi. ~droppings/dung n samadi/mavi ya farasi. horseflesh n nyama ya farasi; (pl) farasi. horsefly n nzi mkubwa (asumbuaye farasi/ ng'ombe). horsehair n manyoya (ya shingo/mkia) ya farasi. horselaugh n kikwakwa, kicheko cha kukwaruza na cha kelele. horseman n mpanda farasi (hasa bingwa). horsemanship n ubingwa wa kupanda farasi. ~meat n nyama ya farasi. ~ play n mchezo wenye ghasia na kelele. horsepond n bwawa la farasi la kuogea na kunywa maji. horsepower n (hp) nguvu farasi. ~ race n mashindano ya mbio za farasi. ~ sense n busara ya kawaida. ~ shoe n njumu/kiatu cha farasi; (kitu) -enye umbo la kiatu cha farasi a ~ shoe desk dawati lenye umbo la kiatu cha farasi. ~ whip n mjeledi/kiboko cha farasi. ~ woman n mwanamke mpanda farasi. horsy adj 1 -a kupenda farasi. 2 -a kuhusu farasi.